Featured Michezo

YANGA YAANZA VYEMA MAPINDUZI CUP 2023

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo_Mzalendo blog

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga SC imeanza vyema katika  Michuano ya Kombe la Mapinduzi CUP 2023 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM mchezo uliopigwa uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Yanga wamepata bao katika  dakika za lala salama 90+5 likifungwa na Dickinson Ambundo

Kwa ushindi huo Yanga wanahitaji ushindi dhidi ya Singida Big Stars ili kutinga hatua ya nusu fainali.

Singida Big Stars wanaongoza Kundi wakiwa na Pointi 3 sawa na Yanga ila wakiwa na uwiano wa kufunga mabao. 

About the author

mzalendoeditor