SIMBA SC imepunguzwa kasi katika mbio za ubingwa baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1_1 na wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba Mjini Kagera.
Kagera Sugar ilianza kupata bao kupitia kwa nyota wao Deus Bukenya dakika ya 15 kabla ya Henock Inonga ajasawazisha dakika ya 38 yaa mchezo na kuwapeleka mapumziko ubao ukisoma 1-1.
Kwa matokeo hayo Simba Sc wamendelea kubaki nafasi ya pili wakiwa na Pointi 38 wakizidiwa pointi 6 na Vinara Yanga wenye Pointi 44.
Michezo mingine iliyochezwa leo Tanzania Prisons wameutumia vyema uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa kuichapa Dodoma jiji mabao 2-0.
Timu ya Geita Gold imeshindwa kutamba katika uwanja wao wa Nyankumbu Girls kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC huku Azam wakibaki nafasi ya tatu akiwa na pointi 37.