Featured Michezo

SIMBA YAICHAPA NAMUNGO FC,YAISHUSHA YANGA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Simba SC imeendeleza na wimbi la ushindi baada ya kuichapa Namungo FC bao 1-0 Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba walipata bao dakika ya 32 likifungwa na Moses Phiri akimalizia pasi ya Mohamed Hussein.

Kwa ushindi huo Simba wameishusha Yanga katika nafasi ya pili mara baada ya kufikisha Pointi 24 wakicheza mechi 11 huku Azam FC wakiendelea kuongoza msimamo kwa Pointi 26 wakicheza mechi 12,nafasi ya tatu inashikiliwa na Yanga wenye Pointi 23 wakiwa wamecheza mechi 9.

Matokeo mengine Timu ya Geita Gold imeng’ara ugenini baada ya kuizamisha mabao 4-2 Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi tatu kupigwa Ihefu watacheza na Polisi Tanzania majira ya saa nane mchana,Mbeya City watacheza na Kagera Sugar majira ya saa kumi jioni.

Mabingwa watetezi Yanga wataikaribisha Singida Big Star majira ya saa moja usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo unaosubiriwa kwa hamu na washabiki na wapenda mpira nchini.

About the author

mzalendoeditor