Featured Kitaifa

EWURA KUTATUA MALALAMIKO YA WATUMIAJI HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  Mhandisi Modeatus Lumato,(kushoto) akiwa katika banda la TANESCO wakati wa Maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa leo Novemba 10,2022.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  Mhandisi Modeatus Lumato, (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika banda la IRUWASA wakati wa Maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa leo Novemba 10,2022.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  Mhandisi Modeatus Lumato,akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja EWURA Kanda ya Kati( kulia) Mhandisi.Martin Maurus na (katikati )ni Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja EWURA Kanda ya Kati wakati wa Maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa leo Novemba 10,2022.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  Mhandisi Modeatus Lumato,(aliyevaa fulana nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa EWURA na wa EWURA CCC katika banda la EWURA alipotembelea banda hilo ili kutoa elimu ya udhibiti kwa wananchi waliotembelea Maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa leo Novemba 10,2022.

…………………………………..

Na .Mwandishi Wetu-IRINGA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),  Mhandisi Modeatus Lumato,amesema kuwa wamejipanga kupokea na kutatua malalamiko ya watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji ili wananchi wapate thamani halisi ya huduma zinazodhibitiwa

Hayo ameyasema leo Novemba 10,2022 wakati akishiriki kutoa elimu ya udhibiti wa huduma katika maonesho ya “Utalii Karibu Kusini 2022” yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa Kilolo, Mkoani Iringa.

 Mhandisi. Lumato amewahakikishia wananchi wa Iringa na mikoa ya jirani kuwa  EWURA ipo kwa ajili yao hivyo kuwataka wawe huru kuwasilisha malalamiko yao kutokana na huduma za umeme, mafuta, gesi na maji.

“Lengo letu ni kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zinapatikana kwa ubora na bei stahiki” ameeleza Mhandisi  Lumato

Aidha, Mhandisi. Lumato ametoa wito kwa EWURA CCC kuendelea kuelimisha wananchi ili wajue haki na wajibu wao wakati wa kupata huduma zinazodhibitiwa.

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inashiriki katika Maonesho ya kuhamasisha utalii wa maeneo ya Nyanda za Juu Kusini yaliyoanza Novemba 9 mpaka  Novemba  12,2022 mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor