Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo Jumapili, Agost 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo
Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.
CHANZO:Mwananchi