Featured Kitaifa

WABUNGE NA WATUMISHI WA BUNGE WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT WATAKIWA KUSAIDIA KUPINGA VITENDO VYA UZEMBE KAZINI

Written by mzalendoeditor

MKUU  wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Paul Simuli,akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo yaliyopewa jina la  Oparesheni  Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi yaliyofanyika  kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

MKUU  wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Paul Simuli,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Mujibu wa Sheria Operesheni Venance Mabeyo Kundi Maalumu la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kanali Erasmus Bwegoge,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Mujibu wa Sheria Operesheni Venance Mabeyo Kundi Maalumu la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi,,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Mujibu wa Sheria Operesheni Venance Mabeyo Kundi Maalumu la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa kikosi cha 834 KJ Makutopora Dodoma Luteni Kanali Festo Mbanga,akitoa taarifa ya mafunzo wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Mujibu wa Sheria Operesheni Venance Mabeyo Kundi Maalumu la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msavatavangu, akisoma risala ya kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT, Oparesheni Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

MKUU  wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Paul Simuli,akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo mara baada ya kufunga Mafunzo ya Mujibu wa Sheria Operesheni Venance Mabeyo Kundi Maalumu la wabunge na watumishi wa bunge  yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora leo Agosti 5,2022 jijini Dodoma.

…………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

MKUU  wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Paul Simuli,amewataka wabunge na watumishi wa bunge wapatao 39 waliohitimu mafunzo kwenda kuisadia serikali kupinga vitendo vya uzembe kazini, rushwa na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazai ya taifa.

Hayo ameyasema leo Agosti 5,2022  wakati akifunga  mafunzo ya awali ya JKT, Oparesheni Jenerali Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi yaliyofanyika kikosi cha 834 KJ Makutopora jijini Dodoma.

Meja Jenerali Simuli amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea vijana  uwajibikaji,uhodari, uzalendo, ukakamavu na stadi za maisha.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa wabunge na watumishi wa bunge mliofanya maamuzi haya ya kizalendo na kijasiri kwa kuacha shughuli zenu na kuja kwenye mafunzo haya mmefanya maamuzi magumu” amesema Meja Jenerali Simuli 

Amesema kitendo cha kuhudhuria mafunzo hayo kunawafanya kuwa wakakamavu, wazalendo, watii na wenye Moyo wa utayari wa kufanya kazi katika mazingira yoyote na nina amini mara baada ya kurudi majimboni utandaji kazi utabadilika.

“Nimepata taarifa kuwa mbali na kujifunza masomo ya darasani na medani pia mmeshiriki katika shughuli za ujasiliamali na tunaamini haya mliyoyapata yatakuwa msaada mkubwa kwenu katika utendaji kazi wenu” amesema.

Amelishukuru Bunge kwa kuwapa nafasi wabunge na watumishi kuhudhuria mafunzo hayo ikiwa ni hamasa kwa vijana kuhudhuria mafunzo hayo na kuzitaka taasisi nyingine kuwapeleka watumishi wao kuhudhuria mafunzo hayo na kujenga uzalendo na mshikamano kazini kwa maendeleo ya taifa.

Hata hivyo, ametumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania kuendelea kujilinda na maambukizo ya UVIKO-19.

“Covid-19 ndugu zangu bado ipo hivyo hatunabudi kuendelea kuchukua tahadhari lakini pia nawashauri kujitokeza kwa wingi kushiriki sensa ya watu na makazi itakayo fanyika mwishoni mwa mwezi huu”amesema

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kanali Erasmus Bwegoge amewashukuru wabunge waliojitoa kupata mafunzo hayo na kuwapongeza wakufunzi wa mafunzo na wanaamini kwa paredi waliyopiga mafunzo hayo yamewaingia.

Amesema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwa wazalendo na wavumilivu katika majukumu yao hasa katika kutunga sheria na katika kuwawakilisha wananchi wao Bungeni.

Awali Mkuu wa kikosi cha 834 KJ Makutopora Dodoma Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kozi hiyo imepewa jina la Oparesheni Generali Venance Mabeyo ili kuenzi kazi nzuri aliyoifanya mkuu wa majeshi ya ulinzi mstaafu.

Amesema kuwa mafunzo hayo yalikuwa ni ya majuma manne ambayo yalianza julai 5 hadi august 5, 2022 yakihusisha watumishi na wabunge 39.

“Katika kozi hii tulikuwa na wanafunzi 39, ambao wote wamemaliza mafunzo wabunge walikuwa 21 na watumishi wa bunge ni 18 ambao tumefundisha, uzalendo, ujasiri, stadi za kazi, usomaji ramani, ujanja wa polini, kufunga na kufungua siraha, mbinu za kivita, ushujaa, kwata,histori ya JKT na JWTZ”amesema

Naye Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msavatavangu, akisoma risala ya kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT, Oparesheni Generali Venance Mabeyo, kundi maalum la wabunge na watumishi,amesema wanapendekeza serikali kutafuta mfumo ambao utatumika kwa wateule wa Rais kupatiwa mafunzo ya JKT, ili kuwasaida kuwa wazalendo na taifa lao na kufanya kazi kwa uadilifu.

“Tunapendekeza bunge kuishauri serikali kuona namna ambayo mafunzo haya tuliyoyapata leo iwe ni kitu cha muhimu kwa wateule wa Rais kukipata ili kuwasaidia kujifunza uzalendo na kulipenda taifa lao”amesema

About the author

mzalendoeditor