Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KUSINI UNGUJA

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma Ripoti ya Utekelezaji wa Kazi za Maendeleo za Mkoa wa Kusini Unguja,kabla ya kuaza kwa ziara yake katika Mkoa huo, taarifa hiyo iliowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Tunguu Wilaya ya Kusini Unguja leo22-7-2022,na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe Masoud Ali Mohamed .

BAADHI ya Watendeji wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mkoa huo wakati ikiwasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadih Rashid , katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tunguu Wilaya ya Kati Unguja 

BAADHI ya Mawaziri na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Maendeleo za Mkoa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Tunguu leo 22-7-2022,kabla ya kuaza kwa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja 

MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wake, kabla ya kuaza kwa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika Wilaya ya Kusini Unguja l

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Wizara ya Afra Zanzibar Said Ali Bakar, akitowa maelezo ya michoro ya Jengo Jipya la Hospitali ya Wilaya Kitogani Wilaya ya Kusini Unguja,  wakati wa ziara yake katika Wilaya hiyo kutembelea Miradi ya Maendeleo, hospitali hiyo inayojengwa kwa Fedha za Uviko-19, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Hafidh Khamis.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kusini inayojengwa Kitongaji kupitia Fedha za Uviko-19, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja leo 22-7-2022, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor