Featured Kitaifa

WAZIRI MASAUNI AAGIZA MAJESHI YOTE NDANI YA WIZARA YAKE KUANZIA SASA YANUNUE VIATU KIWANDA CHA BIDHAA NA NGOZI KILIMANJARO

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), Mjini Moshi, leo Julai 2, 2022. Ameagiza majeshi yote yaliyopo ndani ya Wizara yake kuanzia sasa yanunue viatu vinavyozalishwa na Kiwanda hicho cha umma kwa kuwa ni bora. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KILC, Masoud Omary.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Maduhu Kazi, alipokuwa akizungumza katika Kikao cha Watendaji wa Wizara na Uongozi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), Mjini Moshi,

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiangalia kiatu cha jeshi kinachozalishwa na kilichozalishwa na Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), wakati wa ziara yake katika Kiwanda hicho kilichopo Mjini Moshi, leo Julai 2, 2022. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiangalia begi la ofisi lililotengenezwa na Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), kilichopo Mjini Moshi, leo Julai 2, 2022. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi, na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KILC, Masoud Omary.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Kikao cha Watendaji wa Wizara na Uongozi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), Mjini Moshi, leo Julai 2, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KILC), Mjini Moshi, wakati alipokuwa anawasili kufanya ziara katika Kiwanda hicho leo Julai 2, 2022. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyio, Dkt. Maduhu Kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

About the author

mzalendoeditor