Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO ATEMBELEA KAMPUNI YA KONGANI YA VIWANDA SINO TAN KIBAHA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikilliza Mkurugenzi wa Kampuni ya  Kongani ya Viwanda Kibaha ya  Sino Tan, Bw. Janson Huang, mara baada ya kufanya ziara katika eneo ambalo ujenzi wa viwanda hivyo hufanyika.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili katika eneo ambalo uwekezaji wa viwanda wa Kampuni ya  Kongani ya Viwanda Kibaha ya Sino Tan ujenzi utafanyika.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Pwani kwaajili ya ziara yake kwenye mkoa huo leo Julai 1,2022.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikilliza Mkurugenzi wa Kampuni ya  Kongani ya Viwanda Kibaha ya  Sino Tan, Bw. Janson Huang, mara baada ya kufanya ziara katika eneo ambalo ujenzi wa viwanda hivyo hufanyika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipata picha ya pamoja na Wawekezaji wa viwanda wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda pamoja na baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kibaha mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa viwanda hivyo Kibaha mkoani Pwani.   Eneo ambalo uwekezaji wa viwanda wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda ujenzi ukiendelea .

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungana na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amemtaka muwekezaji wa viwanda wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda kufika katika ofisi za  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuhakikisha Mpango Mkakati wa Tathimini ya Athari ya Mazingira unafanyika katika eneo la viwanda.

Ametoa agizo hilo leo Julai 1,2022 mara baada ya kufanya ziara katika eneo ujenzi wa viwanda mkoani humo ambapo ameipongeza uwekezaji unaofanywa na kampuni hiyo katika eneo hilo.

Amesema licha ya kampuni hiyo kuwa na mkakati mzuri kwenye uwekezaji wa viwanda wilayani Kibaha basi kuna umuhimu wa taratibu wa kuhakikisha anafahamu ni namna gani wanaweza kujipanga kuhakikisha awaathiri mazingira katika shughuli ambayo watakuwa wanafanya.

“Kwa muktadha wa mazingira kwenye eneo hili, inatakiwa ifanyike Mpango Mkakati wa Tathimini ya Athari ya Mazingira, hili ni andiko kubwa ambalo litasainiwa kwenye ofisi yangu, kwakuwa kuna mambo mengi yanakuja huku ni lazima SEA ikamilike haraka iwezekanavyo”. Amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo ametoa maelekezo ndani ya mwaka mmoja Mpango Mkakati wa Tathimini ya Athari ya Mazingira uwe umekamilika ili kuruhusu michakato mingine iiweze kufanyika vizuri katika mazingira yaliyopangwa vizuri katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Kongani ya Viwanda Kibaha ya  Sino Tan, Bw. Janson Huang, amemuwakikishia Waziri Jafo kutekeleza maagizo yote waliyowaelekeza ili kuhakikisha uwekezaji ambao wanaufanya unakidhi matakwa na sheria ya Uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika eneo hilo.

About the author

mzalendoeditor