Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini leo ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Kamishna Jenerali Mstaafu Thobias Andengenye, katika ziara hiyo ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Jenerali Mstaafu Thobias Andengenye pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo, leo.Amewapongeza Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma kwa kazi nzuri wanaoyoifanya katika Mkoa huo na kuwataka kuendelea kusimamia Sheria ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu Thobias Andengenye akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, iliyopo Kigoma mjini leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mst. Thobias Andengenye na Wajumbe wa Kamati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Sudi Mwakibasi.