Featured Kitaifa

WANAWAKE WATAKIWA KUWA WATAFUTAJI WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA NCHI ZAO.

Written by mzalendoeditor

Mbunge viti maalum mkoa wa Mtwara Anastazia Wambura akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wanawake viongozi unaendelea mkoani Arusha.

KATIBU Mkuu wa umoja wa wanawake wa Bunge la jumuiya ya Africa mshariki (EALA) Fatma Ndagiza akiongea na waandishi wa habari katika mkutano.

Mmoja wa wanaharakati wanaopigania haki za wanawake kutoka Congo DRC  Agnes Sadiki ambaye pia alishawahi kuwa waziri wa uchukuzi nchini humo, msemaji wa serikali na waziri wa bajeti akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha.

Dkt Rebecca Kadaga waziri wa jumuiya ya Africa mashariki kutoka Uganda akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.

PICHA ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa wanawake viongozi unaoendelea mkoani Arusha.

………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Wanawake kutoka nchi mbalimbali za Kanda za Afrika ikiwemo EAC, SADIC, COMESA na ECOWAS wametakiwa kuwa watafutaji wa nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi zao lakini pia jamii kuhakikisha wanawake wanapata nafasi  zikiwemo za kisiasa.
Wito huo umetolewa na Anastazia Wambura  mbunge wa viti maalum mkoa wa Mtwara wakati akifungua mkutano wa wanawake viongozi wanawake unaoendelea mkoa Arusha katika makao ya jumuiya ya Africa mshariki kwa niaba ya spika wa spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ambapo alisema kuwa ni vema wanawake wakapata nafasi za uongozi kwani mwanamke ndiye mzazi,mlezi, mtu mwepesi wa kubaini matatizo katika jamii pamoja na chombo kikubwa Cha amani.
Alisema wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazozuia wao kuingia katika nyanja za siasa/uongozi ikiwemo kukabiliwa na shughuli nyingi za kifamilia hivyo katika mkutano huu watajadili changamoto hizo na namna bora ya kuweza kukabiliana nazo.
“Mambo mengine ni Mila, desturi na tamaduni ambazo zinawaona wanawake ni viumbe duni ambao hawawezi kutoa maamuzi kwahiyo mambo kama haya ndo yanaenda kujadiliwa lakini pia kubadilishana uzoefu kati ya nchi na nchi kuona wao wamewezaje kwa mfano Rwanda utaona wao wako karibia asilimia 64 ya wabunge ni wanawake lakini kwetu Tanzania ni asilimia 37  na wapo ambao wapo chini ya hapo hivyo tutabadilulishana uzoefu,” Alisema.
“Tutaangalia kwa pamoja tufanye nini ili tuweze kuhakikisha kwamba wanawake Afrika wanapata nafasi za uongozi kwani tunataka tuwe asilimia 50 kwa 50 lakini kwasababu ya hizi changamoto ndio maana bado hatukafikia lakini pia ni nafasi za wakereketwa kuhakikisha kwamba nafasi za wanawake zinaongezeka, bado nchi nyingi hazijawaweza kuweka kwenye mitaala lakini ni mapendekezo,” Alisema.
“Kwamba watoto wanapoingia darasa la kwanza hadi lasaba wajue kuwa mwanamke ni mtu wa muhimu katika kuiendeleza jamii kwahiyo wasiwe na mtadhamo hasi dhidi ya mwanamke, watakapowekewe kwenye mtaala moja kwa moja akiwa mkubwa akiambiwa nenda kapige kura anakuwa akijua niliambiwa kuwa mwanamke ni kiumbe muhimu katika kuleta maendeleo kwenye jamii,” Alieleza.
Kwa upande wake Dkt Rebecca Kadaga waziri wa jumuiya ya Africa mashariki kutoka Uganda alisema kuwa amekuwa spika wa Bunge la Uganda kwa miaka kumi hivyo yupo katika mkutano huo kubadilishana uzoefu nini wafanye ili wanawake waweze kupata nafasi za uongozi ikiwemo kukagua mambo mbalimbali ya serikali ikiwemo bajeti na uwakilishi wa wanawake kwa kuhakikisha asilimia 30 wanashiriki.
“ Tunataka kuhakikisha kuwa katika maeneo yetu kunakuwa na shule sahihi kwaajili ya watoto wa kike kwahiyo tupo kushauri kuhakikisha tunapaza sauti kwa pamoja na kufikia malengo ya kidunia katika nchi zetu za kuleta usawa katika mambo mbalimbali ikiwemo nafasi za uongozi,”Alisema.
 mmoja wa wanaharakati wanaopigania haki za wanawake kutoka Congo DRC Agnes Sadiki ambaye pia alishawahi kuwa waziri wa uchukuzi nchini humo, msemaji wa serikali na waziri wa bajeti alisema kuwa amefurahi kuona nchi nyingi zinaendea kupiga hatua katika kuwashirikisha mwanamke katika ngazi za uongozi na kutolea mfano Tanzania Zambia na Rwanda.
“Itatubidi katika nchi yetu ya Congo kuomba wakuu viongozi ambao nao wamesaini mikataba mbalimbali ikiwemo ya protocoli ya MAPUTO na nyinginezo ambazo zinaomba kumshirikisha mwanamke katika kila kitu ambacho kina lenga amani kwasababu hakuna uongozi bila amani lakini pia katika chaguzi kwani Congo tunajitahidi kuwa nchi yenye demokrasia,” Alisema.
“Tutaenda katika uchaguzi hivi karibuni kwahiyo ni sharti  wakuu viongozi kama walivyosaini ile mikataba  na kukubaliana kumweka mwanamke katika ngazi ya uongozi waweze kuzitekeleza lakini inabidi pia wanawake wao wenyewe wafanye juhudi za kuingia katika uongozi kwani wanastahili kuongoza pamoja na wanaume lakini pia watambue kuwa hawataweka tu kwa sababau ni wanawake bali wawe wanawake wanaostahili,” Alisema .
“Wawe wanawake wenye ujuzi, wasomi, wamelimika lakini vilevile awe na jitihada ya yule ambaye anastahili kuongoza kwa niaba ya wananchi kwa faida ya akina mama na raia wengine,” Aliongeza.
Naye katibu mkuu wa umoja wa wanawake wa Bunge la jumuiya ya Africa mshariki (EALA) Fatma Ndagiza alisema kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo ni kuwapa nafasi wanawake waliopo katika siasa nafasi  na kubadishana mawazo na uzoefu hasa jinsia gani walifika katika nafasi walizonazo zinazotoa uamuzi,  kuelezana changamoto na ninamna gani wataweza kuzikabili changamoto hizo.
“Tunatarajia kuwa baada ya mazungumzo haya tutakuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo ya kujitahidi kubadili Katiba za nchi zetu au kama wawakilishi tuweze kufuatilia na kuhoji serikali zetu ili wanawake wawe na mchango  kwa maendeleo ya taifa zao lakini pia wawe na wanawake wengi katika ngazi za siasa,” Alisema.

About the author

mzalendoeditor