Featured Michezo

UONGOZI WA WIZARA WAITAKA TEMBO WARRIORS KUTUMIA MECHI ZA ULAYA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA, WAIAGA RASMI LEO

Written by mzalendoeditor

 

Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na michezo.Mhe, Mohamed Mchengerwa ameitaka Timu ya
soka ya walemavu ya (Tembo Warriors) kutumia mechi za maandalizi na
nchi mbalimbali za Ulaya kujinoa ili kushinda kombe  hilo na kulirejesha
nchini.
Mhe
Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2022 uwanja wa Benjamini Mkapa
wakati akiikabidhi bendera ya Taifa timu hiyo akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi inayokwenda kuanza kucheza mashindano
kwenye maandalizi na timu  mbalimbali za Ulaya kwa kuanzia na timu ya
Poland ili kuweza kupata uzoefu wa kucheza na nchi za mabara mbalimbali 
kabla ya kuanza mashindano haya.
“Tumeamua
kama Serikali kuendelea kuhaakikisha kuwa tunazisaidia timu zinazofanya
vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ili kuwasaidia kukuza ajira na
kuwafanya  waajiriwe  kwenye vilabu  vikubwa  duniani” amefafanua Mhe.
Mchengerwa 
Amesema
watanzania wamechoka kuona kuwa nchi inasuasua kwenye michezo na
amesisitiza kuwa  wakati huu watanzania wanataka  kombe  la dunia kuja 
Tanzania ambapo amesema  hilo litafanikiwa kwa kuweka mbele utaifa na
uzalendo wanapokuwa kwenye mashindano haya.
Ameongeza
kuwa jambo kubwa kwa sasa ni kuwa na nidhamu na kuzingatia misingi
ambayo wanapewa na  makocha wa timu zao ili waweze  kufika mbali na
kuboresha  maisha yao na uchumi wan chi yetu kwa ujumla.
“Naomba
kuwaambia mkifanya vizuri katika mashindano  haya ya maandalizi tu nina
uhakika  mtanunuliwa na timu kubwa na mtabaki ulaya, mtabadilisha
maisha ya familia zenu na watanzania kwa ujumla” ameongeza Mhe.
Mchengerwa
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti  viongozi wa timu hiyo  wamemwahidi Rais wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania kuwa wanakwenda  kuanza kutema cheche  katika
maandalizi ya timu hizo za awali ili kujihakikishia  kutwa kombe hilo.
Katibu
Mkuu. Dkt, Abbasi amesema  Tembo Warriors ndiyo timu ya kwanza nchini
kufuzu kuingia kwenye mashindano hayo na kuitaka kuendelea kushikilia
heshima  hiyo kwa kuwa timu ya kwanza kurejesha kombe  nyumbani.

About the author

mzalendoeditor