Featured Kitaifa

DC TANGA:WAFANYAKAZI NI MIONGONI MWA WAHANGA WAKUBWA WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA, AIPONGEZA CRDB KWA SIKU YA WELLNESS DAY

Written by mzalendoeditor

MKUU
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa siku ya
Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni
maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa
ni kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi kushoto ni Meneja wa
Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa ,Mkuu wa wilaya ya Muheza
Halima Bulembo na kulia ni Meneja wa CRDB Tanga January

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa siku ya
Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni
maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa
ni kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi kushoto ni Meneja wa
Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa ,Mkuu wa wilaya ya Muheza
Halima Bulembo na kulia ni Meneja wa CRDB Tanga January

Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa na kushoto ni Mkuu wa wilaya
ya Muheza Halima Bulembo

Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MKUU
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amesema miongoni mwa wahanga
wakubwa wa magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Presha na Kisukari na
mengine ni wafanyakazi kwa sababu siku zote wamekuwa na maisha
yanayotabirika.

Mgandiliwa aliyasema hayo wakati wa siku ya
Wellness Day iliyoanzishwa na Benki ya CRBD ikiwa ni maalumu kwa ajili
ya wafanyakazi kushiriki katika michezo lengo likiwa ni kutafakati na
kuthamini mchango wa wafanyakazi .

Ambapo waliona ni bora
waanzishe siku hiyo maalumu ya kuwasaidia na kuleta furaha kwa
wafanyakazi na kuona jinsi gani wanaweza kuweka uwiano sawa kati ua
maisha ya kazi na maisha binafsi ili kazi isijekuwa adhabu

Umuhimu
wa siku hiyo unatokana na kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa siku zote
365 kasoro siku ya Krismas na Eid kwa kutokana na hilo benki hiyo
ilikuja ikafikiria, kutafakati na kuthamini mchango wa wafanyakazi na
kuona bora ianzishe mpango huo.

Alisema kwani asubuhi wanaingia
kazini wakimaliza wanakula na kulala na siku inayofuatia wanaendelea na
kazi hivyo maisha yao yana mzunguko huo kupitia huko miili inakuwa
dhaifu sana kinga zinakuwa zimeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na
aina ya maisha wanayoishi.

“Leo hii magonjwa kama
vile Presha,Kisukari yanaongezaka kwa kiwango kikubwa tatizo hatufanyia
mazoezi..ukiona mtu anaamka asubuhi anaenda ofisini muda wa kula
anaondoka na akirudi anaendelea na shughuli zake na mwisho wa siku
hawana muda ma mazoezi anatoka ofisi wanarudi nyumbani wamechoka anaoga
anakula na kulala”Alisema DC Mgandilwa.

Mkuu huyo wa wilaya
alisema jambo ambalo wamelifanya kwake ni sehemu ya shughuli ndani
hivyo isipokuwa kuna maboresho wanatakiwa kuyafanya wakati mwengine .

“Niwaambie
tu kwamba idara iliyoratibu sio vibaya wakaendelea kwenye matawi yao
kwa kuweka vyumba vya mazoezi kuwawezesha wafanyakazi waweze kushiriki
kwenye mazoezi lakini tofauti na hapo tutaishi kukuta na na kutimiza
wajibu”Alisema DC Mgandiliwa.

Hata hivyo alisemaq benki hiyo
imekuwa mmoja wa wabia wakubwa sana wa Serikali kwa kujitolea hivyo nao
wataendelea kuwahaidi kuwa kushirikiana nao bega kwa bega ikiwemo
kuendelea kufungua milango

Awali akizungumza Meneja wa Kanda ya
Kaskazini wa Benki ya CRDB Chiku Issa alisema Siku ya Wellness Day ya
Benki hiyo ilianzishwa miaka miwili iliyopita bahati mbaya watu wa Kanda
ya Kaskazini wanaifanya kwa mara ya kwanza kwa sababu hapo nyuma
walishindwa kutokana janga la Corona.

Alisema walipoanza kanda
hiyo walilazimika kuigawa mara mbili kwa sababu za kijografia na ya
kwanza ilifanyika Mkoani Arusha iliyoshirikisha wafanyakazi
Manyara,Arusha na Kilimanjaro.

“Tuliona tuigawe mara mbili leo
tupo hapa Tanga kwa ajili ya siku hii tupo kuangalia afya na wafanyakazi
wa benki kama mnavyojua tunaingia kazini lakini muda wa kutoka hatuna
mpaka tuhakikishe vitabu vimebalance ili kuweza kujianda na siku
inayofuata”Alisema Meneja huyo wa Kanda ya Kaskazini.

Naye kwa
upande wake Meneja wa Rasiliamali Watu wa Benki hiyo wa Kanda ya
Kaskazini Cosmas Sadat alisema Tanga wana malengo yao wanaamini kwamba
mkoa huo unaweza kuwa Hub ya Kanda ya Kaskazini .

Alisema
wamefanya mabadilko madogo ya kuhamisha wafanyakazi kwa ajili ya
kuchanganya wanatengeneza ili ziweze kuwa na uwiano sawa na wanataka
kila mkoa nguvu zilingane kwa kufanya hivyo kanda hiyo wataweza kuwa wa
kwanza.

About the author

mzalendoeditor