Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA AZINDUA MRADI WA BOOST WA KUIMARISHA UJIFUNZAJI SHULE ZA MSINGI.

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mradi wa boost hafla iliyofanyika leo Juni 6,2022 jijini Arusha.

Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mradi wa boost hafla iliyofanyika leo Juni 6,2022 jijini Arusha.

MWAKILISHI wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Ms Mara Warwick,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mradi wa boost hafla iliyofanyika leo Juni 6,2022 jijini Arusha.

WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Arusha wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa mradi wa boost 

 WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda kulia akishikana mkono na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Ms Mara Warwick baada ya  kuzindua mradi wa boost uliofanyika Leo Juni 6,2022 mkoani Arusha.

……………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amezindua  mradi wa kuimarisha ujifunzaji shule za msingi na awali uliofadhiliwa na benki ya Dunia kwa shilingi Trilioni 1.15.
Akizindua mradi huo Leo Juni 6, 2022 Mkoani Arusha Prof. Mkenda alisema utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano  utaboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufunfishaji, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za utoaji huduma ngazi A halmashauri.
“Katika maeneo haya matatu program itajikita katika afua mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kuzingatia mahitaji hususan ujenzi wa madarasa, uimarishaji wa mpango wa shule salama, kuimarisha uwiano wa uandikiswaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, kuboresha vifaa na njia za ufundishaji elimu ya awali, pamoja na kuimarisha na kuendelea mpango wa mafunzo ya walimu kazini,” Alisema Profesa Mkenda.
“ Pia utaimarisha vituo vya elimu ya msingi katika mtaala wa TEHAMA  na kuendelea utendaji wa bajeti kwaajili ya shughuli za elimu na kuendeleza utawala bora katika elimu, ambapo madarasa  12000 yatajengwa nchi nzima kwa miaka mitano kwa kila mwaka kujenga madarasa 3000 na afua zote zitatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo(EP4R),” Alieleza.
Alifafanua kuwa pia kupitia mradi huo wa boost shule 6000 nchi nzima zitatekeleza mpango wa shule salama, vituo vya walimu na shule za msingi 800 kiwekewa vifaa vya TEHAMA kwaajili ya kuwawezesha walimu kujifunza na utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu , madarasa 12000 ya Elimu ya awali kuboresha, uandikisha wa wanafunzi elimu ya awali kuongezeka.
Aidha aliwasihi watendaji wote kutoka ngazi ya wizara na taasisi watakaohusika na utekelezaji  wa mradi huo kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuhakikisha serikali inafikia vigezo na viwango vyote vilivyowekwa kila mwaka kwani kadiri watakavyokuwa wanatekeleza ndio fedha zitakavyokuwa zinaletwa ambapo wakitekeleza kwa kusuasua fedha zitaletwa kwa kusuasua.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Ms. Mara Warwick  alisema kuwa boost itasaidia serikali katika maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuhakikisha elimu ya awali na msingi inawafikia watoto wote katika shule za serikali ambapo benki ya Dunia inatarakia mradi huo utawafikia watoto zaidi ya milioni 12 nchini Tanzania.
Pia alisema kuwa manufaa ya mradi huo ni makubwa kwa kizazi kinachokuwa na watanzania wote ambapo pia aliipongeza serikali kwa kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa elimu kwa kuwaruhusu wanafunzi walioshindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari kwa sababu mbalimbali kurudi mashuleni kurudi shule na kuweza kupata elimu mapema mwaka huu.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI David Silinde alisema kuwa wizara yake ndio watekelezaji wakuu wa mradi huo ambapo wamepokea tangu wakati wa maandalizi hivyo watasimamia utekelezaji wake kwa kuzingatia vigezo vya utendaji ambapo wamejipanga kuwajengea uwezo wasimamizi wa mradio huo.
Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge inayojihusisha na masuala ya huduma na maendeleo ya jamii Aloyce Kamamba ameishukuri serikali kwa kuanzisha mradi huo lakini kutokana na walimu kufanya kazi kubwa ni vema ikaajiri walimu watakaokuja kuwahudumia watoto kwani miundombinu na walimu inaenda sambamba.
Naibu katibu mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Charles Msonde  alisema kuwa serikali imeendelea kupata mafanikio katika kuboresha sekta ya elimu kutokana na mpango waliojiwekea katika afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ufaulu katika mtihani wa darasa la saba kutoka asilima 77.7 mwaka 2018 na kufikia asilimia 81 mwaka 2021.
Kamishna wa Elimu kutoka wizara ya Elimu sayansi na teknolojia Dkt Lyabwene Mtahabwa alisema kuwa elimu ya awali na msingi ndio msingi hasa wa makuzi ya mtoto ambapo tabia zote nzuri na muhimu mtoto anazipata na kupitia mradi huo wataweza kupata na mradi huo ulitokana na changamoto zilizobainika katika uchambuzi wa taarifa za sekta ya elimu 2021ambazo sinaathiri utoaji wa elimu bora katika ngazi za elimu msingi.

About the author

mzalendoeditor