Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Maunt Meru alipowasili Kuzungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha katika Ziara yake ya Kujitambulisha pamoja na Kukagua Uhai wa Chama mkoani humo,
Mwanachama akiwa amenyanyua Bango la Kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipowasili Kuzungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha katika Ziara yake ya Kujitambulisha pamoja na Kukagua Uhai wa Chama mkoani humo
Shamra Shamra za Wanachama wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Mara baada ya Kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipowasili Kuzungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha katika Ziara yake ya Kujitambulisha pamoja na Kukagua Uhai wa Chama mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo Katia mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo katika Ukumbi wa Maunt Meru.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa Itikati na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka , Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Stephen Zelote,
Katibu wa Itikati na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akipepelusha bendera waakt akiongoza Wanachama wa CCM kuimba nyimbo za Hamasa kaaika Mkutano hou.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Wana Chama wa CCM Mkoa wa Arusha katika Mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana e ya Kujitambulisha pamoja na Kukagua Uhai wa Chama mkoani humo, Leo. Aprili 27, 2022.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akivishwa na kukabidhiwa baadhi ya Vitu Vywa Kiasili katika kabila la Kimasai kama Ishara ya Kusimikwa kuwa Kiongozi wa Juu wa Kabila Hilo na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Ndg Lekule Laiza
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza na Maelfu ya Wanavchama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Ukumbi wa Maunt Meru katika Ziara yake ya Kujitambulisha pamoja na Kukagua Uhai wa Chama mkoani humo, Leo. Aprili 27, 2022. (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI WA CCM)
………………………………
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ametoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha wote waliotajwa kufuja fedha za umma kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) wanachukuliwa hatua.
Amesema haina maana kila mwaka ripoti ya CAG inatolewa halafu hakuna hatua ambazo zinachukuliwa dhidi ya wahusika wote ambao wametajwa, hivyo umefika wakati sasa kuchukua hatua ili kukomesha ufujaji wa fedha za umma.
“Kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kinyume na utaratibu, niwoambe wenzangu serikali, ni wakati muafaka watu waliotajwa, waliohusika, waliotenda, walioshiriki kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua.
“Kila mwaka ripoti ya CAG inapotolewa wabunge wamekuwa wakijadilia na baada ya kujadili inakuwa nini? Haitoshi hatua zikichuliwa hali inakuwa tofauti , wabunge wanazungumza kwa ukali kabisa, taarifa inaandika halafu inakuwa imekwisha.
“Mwaka unaofuata mambo ni yale yale, wizi ni ule ule, ingekuwa hatua zinachukuliwa papo kwa papo haya mambo yangeisha.Watu wangechukua wanachukuliwa hatua wangechukua tahadhari, waliohusika waondolewe na watu wa kujaza hizo nafasi wapo.
“Wakati umefika kwa Serikali kufanyia kazi kwa kina ripoti ya CAG ili wananchi waridhike mali ya umma haitumiki vibaya.Mnaunga mkono au tuwahurumie, haiwezekani vitabu vya CAG vinaandikwa kila mwaka hali inakuwa hivyo hivyo , lazima tuchukue hatua, uamuzi wa kuagiza serikali sina lakini uwezo wa kushauri ninao,”amesema Kinana.
Ameongeza kuwa bahati nzuri yeye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM na kazi zake ni mbili tu , mosi kukaa kwenye kiti cha mwenyekiti iwapo hayupo na kawaida mar azote mwenyekiti anakuwepo na kazi ya pili ni kumshauri mwenyekiti na kusema yale ambayo Mwenyekiti amemuagiza.
“Ukiona nasema basi Mwenyekiti mwenyekiti kanituma, hivyo hamtanishataki, hivyo nayosema nasema kwa niaba yake.Nawashauri waliohusika kwenye ripoti ya CAG hatua zichukuliwe, ili fedha za wananchi zisichezewe na wengi waliotajwa huko ndani wamekula kiapo cha uadilifu, hivyo natoa mwito huu kwa vyombo vya serikali.
“Nimeagiza kistaarabu tunatoa ushauri, hata hivyo kikao cha chama ndicho kinachoweza kutoa maagizo.Nashauri jambo hili lakini nina nafasi ya kumshauri Mwenyekiti wangu ili hili jambo likapate baraka ya vikao,”amesema.
Kinana amewataka watendaji na wafanyakazi kutosubiri maelekezo ya Rais.” Si kila jambo lazima Rais aagize.. tujenge utamaduni wa kuwajibika sisi wenyewe”