Featured Kitaifa

KINANA ATEMA CHECHE MKOA WA PWANI

Written by mzalendoeditor
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Mkuranga katika Ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi  Mkoani Pwani
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akifungua kitambaa ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi la CCM Mwanambaya Wapili kulis bi Amina Ndomboroke Mwenyekiti wa Shina hilo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akipanda mti  mara baada ya  kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi CCM Mwanambaya
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana , Akifurahi pamoja na kikundi Cha Hamasa na Itifaki Wilayani Mkuranga  alipowasili katika Ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi  Mkoani Pwani
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mio wa Pwani, Ramadhani Maneno baada ya kuwasili patika ofisi za CCM Wilaya ya Mkuranga.
Makamu Mwenyekiti wa wa CCM Tanzania Bara, Ndg Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno wakiwa katika kutano wa ndani wa Chama wilayani Mkuranga.
Viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wakisimama kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM alipowasii katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya montano wa ndani wa Chama wilayani Mkranga.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wana CCM katika mkutano wa ndani alipofanya ziara ya kujitambulisha mkoani Pwani. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mkuranga
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Makamu mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzungumza na Wana chama wa Mkuranga.
…………………………
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amewataka  viongozi wa ngazi zote kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru, haki na wenye kuzingatia katiba ya CCM na kanuni zake ili kuwapata viongozi waadilifu.
Pia amewataka wana-CCM kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi ndani ya Chama katika uchaguzi unaoendelea.
Kinana ametoa kauli hiyo leo  24 Aprili 24,2022 wakati wa ziara yake katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ya uimarishaji uhai wa chama na kuhamasisha wana-CCM kujitokeza kushiriki uchaguzi wa ndani ya Chama unaoendelea.
 
“Viongozi simamieni uchaguzi uwe huru na haki, acheni kubeba wagombea, epukeni dhulma na chukueni hatua kwa kuwakata wale wanaotafuta uongozi au umaarufu kwa fedha. Kwa kuwa tunataka uadilifu nje ya CCM basi ni lazima tuanze kwanza sisi kuwa waadilifu.” Amesema Kinana
 
“Wana-CCM wanayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa lakini haipo haki ya kununua au kununuliwa ili kupata au kutoa uongozi.  Kuna watu huwa hawana habari na chama wala wanachama wakati ambao sio wa chaguzi ajabu wakisikia uchaguzi tu wanaanza kujipitisha kuwasalimu, kugawa fedha na kuwachafua wengine tusiruhusu haya yajitokeze.”
 
Aidha Kinana amesema mahusiano mazuri baina ya CCM na serikali ni chachu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM hali inayoimarisha imani ya wananchi kwa Chama na serikali yao. Pia amewataka viongozi wa CCM kuendeleza utamaduni wa kuwasikiliza wananchi na kuwasilisha changamoto zao serikalini kwa utatuzi. Amehimiza wajibu huo ni walazima kwa sababu ni CCM inayoomba kura na inayopigiwa kura.
 
Aidha Kinana ameshiriki uzinduzi wa ofisi ya tawi la Mwanambaya kata ya Mipeko wilaya ya Mkuranga ambapo alichangia shilingi milioni tatu kuunga mkono juhudi za Wana-CCM na viongozi wa tawi hilo za kupata mazingira mazuri ya kufanyia shughuli za Chama. 
 
Katika ziara hii viongozi walioshiriki ni pamoja na mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg Ramadhani Maneno, Kamati ya siasa ya mkoa wa Pwani, kamati za siasa za wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndg Abubakar Kunenge, wakuu wa wilaya zote, watendaji wote, wabunge na madiwani wote wa Mkoa wa Pwani. Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana ameondoka mkoa wa Pwani kuelekea mkoa wa Tanga kuendelea na ziara yake akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka. 

About the author

mzalendoeditor