Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AKEMEA VITENDO VYA KUWAFICHA WENYE MAHITAJI MAALUM

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturu na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Buigiri  wilayani Chamwino, Dodoma ambacho kinamilikiwa na Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Central Tanganyika,  Aprili 21, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania wenye tabia ya kuwaficha watoto  Wenye Ulemavu kuacha mtindo huo badala yake wahakikishe wanawapa fursa ya kupata elimu.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Aprili 21, 2022) alipofuturu na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Buigiri, Wilayani Chamwino ambacho kinamilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika.

Amesema kuwa ili kuhakikisha watoto hao wanapata Elimu, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mahitaji mbalimbali kwa ajili kujifunza na kufundishia

Naye, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamisi amesema kuwa tukio hilo ni ishara ya upendo wa viongozi wakuu wa Serikali kwa kundi la watu wenye mahitaji maalum

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani ameshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa uamuzi wake wa kuamua kula futari na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Buigiri, Wilayani Chamwino

Aidha Askofu Dkt. Chilongani amemuhakikishia Waziri Mkuu kuwa Kanisa hilo linaendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Sita katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kudumisha amani.

About the author

mzalendoeditor