Featured Kitaifa

LAAC YAUSHAURI UOGOZI WA SHULE YA SAJO KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Na Asila Twaha, Misungwi

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Zedi ameushauri uongozi wa shule ya sekondari Sanjo kuendelea kushirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo ya elimu katika maeneo wanayoishi.

Mhe. Zedi ametoa wito huo tarehe 21 Machi, 2022 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambapo walikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Jengo la Utawala na Shule ya Sekondari Sanjo iliyopo Kata ya Usagara na kuridhishwa na miradi iliyokuwa inaendelea na ujenzi katika Halmashauri hiyo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa vyumba 3 vya maabara vilivyokamilika vikiwemo na vifaa vya kujifunzia Mkuu wa shule hiyo Mwl. Emmanuel Kulwa amesema, mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya maabara ulipokea fedha kutoka Serikali Kuu shilingi milioni 60 na shilingi milioni 54 ni nguvu ya wananchi.

Amefafanua kuwa lengo la mradi wa ujenzi wa maabara ni kuongeza ufaulu wa masomo ya sayansi ambapo hapo awali vifaa vya maabara vilikuwa vikihifadhiwa stoo na wakati wa kujifunza vifaa hivyo huhamishiwa darasani hali iliyopelekea kuwa na mazingira magumu ya kufundisha na kujifunzia na wakati mwengine vifaa hivyo huaribika kwa sababu ya kuvihamisha kila mara.

“Mwaka 2021 watahiniwa wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi ni 301 watoto 64 walifaulu vizuri 100%” amesema Mwl. Kulwa

“kukamilika kwa maabara hiyo kumesaidia kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi lakini pia wanafunzi hao kwa sasa wanajifunza kwa nadharia na vitendo lakini pia uharibifu wa vifaa umepungua sababu vimewekwa sehemu salama” amesema Mwl. Kulwa

Mhe. Zedi ameupongeza uongozi wa shule ya Sekondari Sanjo na kutoa wito kwa walimu kutumia maabara hiyo kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi ili Taifa liwe na wataalam wakutosha.

About the author

mzalendoeditor