Uncategorized

CCM KILOLO KUANDIKA HISTORIA MPYA

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa
chama wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo Kiliani Myenzi kushoto akiangalia namna ambavyo ujenzi wa ofisi ya chama hicho ambayo wanatarajia itakuwa ofisi ya mfano kwa wilaya nyingine za kichamaMwenyekiti wa halmshauri ya wilaya
ya Kilolo Anna Msolla akiwa anafanya usafi katika jengo
linalojengwa kuwa ofisi ya CCM wilaya ya kilolo.Viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa na wanachama pamoja na wadau wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiangalia mwenendo wa ujenzi wa ofisi ya chama hicho

katibu wa Itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo Remy Sanga akiwa anafanya usafi kwenye eneo la ujenzi wa ofisi mpya za ccm kilolo.

 

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapinduzi wilaya ya kilolo kimesema kinajenga
ofisi ya chama ya mfano nchini mzima kwa namna ambavyo wametumia michoro bora na
ya viwango vya juu.

Akizungumza na waandishi wa habari,mwenyekiti wa
chama hicho Kiliani Myenzi alisema kuwa walianza mchakato huo muda mrefu kwa
kuhakikisha kuwa wanajenga jingo la ofisi hiyo kwa viwango vya kimataifa.

Myenzi alisema kuwa lengo la kujenga ofisi hiyo mpya
ni kuhakikisha watumishi wa chama wa chama hicho wanafanya kazi katika ofisi
yenye ubora na kuongeza ufanisi wa kazi zao kulingana na ofisi wanayofanyia
kazi.

Alisema kuwa CCM kilolo imekuwa inawanachama wengi
wanaokipenda chama hicho hivyo lazima wajenge ofisi ambayo inaendana na uchumi
wa wilaya hiyo ambao wananchi wake wamekuwa wanajituma kufanya kazi.

Myenzi alisema kuwa ofisi hiyo inatarajiwa kukamili
hivi karibuni kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda kwa kasi kubwa na kwa asilimia
kubwa kila kitu kimekamili bado umaziaji tu.

Alisema karibu na ofisi hiyo pia utajengwa ukumbi
mkubwa wa kisasa kwa ajili ya mikutano na sherehe mbalimbali ambapo pia utakuwa
ukumbi wa mfano kwa mkoa wa Iringa.

Myenzi alisema kuwa ukumbi huo utakuwa fahari kwa
wananchi na wanachama wa wilaya ya Kilolo na nje ya wilaya ya Kilolo kwa wale
ambalo watakuwa wakiutumia kwa shughuli mbalimbali.

Alisema kuwa
katika kufanikisha ujenzi huo hawezi kuacha kuwashuku wadau mbalimbali
waliochangia ujenzi huo kama vile MNEC Salim Abri Asas,mkuu wa wilaya aliyepita
Asia Abdalah,wakurugenzi,wabunge wastaafu na wadau wengine ambao hawajatajwa
hapo juu.

Myenzi alimalizia
kwa kusema ofisi na ukumbi vikikamilika ndio itakuwa alama yake katika
kuwatumikia wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo kwa
kipindi akiwa mwenyekiti wa chama hicho.

Alisema kuwa
anatarajia kugombea tena nafasi hiyo wakati ukifika kwa kuwa bado anamatarajio
mengi ya kuisaidia wilaya ya kilolo kupata maendeleo na kukuza uchumi wa
wananchi wa wilaya hiyo.

Kwa upande
wake katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo Remy Sanga alisema kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo pamoja na ukumbi kutaongeza kasi ya
ufanisi wa kazi kwa watumishi wa chama hicho.

Sanga alisema kuwa
ukumbi ukikamilika kwa wakati na ubora ambao wanautarajia basi kitakuwa moja ya
vitega uchumi vya chama hicho wilaya ya Kilolo.
Aaliwaomba
wadau mbalimbali kuendelea kuchangia ujenzi wa ofisi na ukumbi huo ili
vikamilike kwa wakati maana ujenzi huo kwa asilimia kubwa unawategemea wadau na
wanachama wa chama hicho.

Sanga alimalizia
kwa kuwaomba wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wote nchi nzima.
 

About the author

mzalendoeditor