Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AREJEA NCHINI NA NEEMA KWA WATANZANIA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.

Sehemu ya Wananchi wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022. PICHA NA IKULU

……………………………………………………..

Na.Alex Sonna,DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amerejea nchini leo baada ya kumaliza ziara ya siku 10 katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji.

Akizungumza na wakazi wa Dar Es Salaam waliojitokeza kumlaki kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal I), Rais Samia amesema ziara hiyo imekuwa yenye mafanikio makubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, uchumi na kutanua sekta nyingine mtambuka za maendeleo.

Pia, Rais amesema mikataba yote iliyosainiwa na misaada ya kifedha iliyopatikana italeta tija kubwa katika kuchechemua shughuli za maendeleo.

Rais amedokeza kwamba wawekezaji kutoka mataifa ya Ufaransa na Ubelgiji watafika nchini Tanzania kumulika na kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo.

Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi amekuwa ziarani kwa siku 10 katika ziara inayotajwa kuwa yenye mafanikio makubwa katika mkondo wa kidiplomasia na kiuchumi.

About the author

mzalendoeditor