Featured Michezo

CHICO USHINDI MAJANGA YAMKUTA, AONDOLEWA YANGA

Written by mzalendoeditor

Mchezaji wa Kimataifa kutoka nchini Congo  Chico Ushindi, atakaukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuumwa ghafla.

Kwa mujibu wa Daktari wa Viungo wa Yanga, Mtunisia, Youssef Ammar, amesema kiungo huyo alipata maumivu ya misuli siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Biashara United uliochezwa juzi Jumanne.

Ammar alisema kuwa Chico alikuwepo katika mipango ya kucheza mechi hiyo ya juzi, lakini maumivu aliyoyapata yalisababisha aondolewe kikosini.

“Kuondolewa kwake kuliharibu mipango ya kocha, hivyo kutokana na maumivu hayo aliyoyapata, atatakiwa kukaa nje ya uwanja kuanzia siku saba hadi kumi kwa ajili ya kupatiwa matibabu, hivyo huenda akaukosa mchezo ujao wa ligi dhidi ya MtibwaSugar,” alisema Ammar.

Vinara hao wa Ligi Kuu ya NBC wanatarajia kucheza na Mtibwa Sugar Februari 25,2022 katika uwanja wa  Manungu, Turiani mkoani Morogoro na utakuwa mchezo wa kufunga mzunguko wa kwanza.

About the author

mzalendoeditor