Featured Michezo

KOCHA PABLO AACHIWA MSALA WA BERNARD MORRISON SIMBA

Written by mzalendoeditor

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco kuamua hatma ya kiungo msumbufu Bernard Morrison kutoka na mkataba wake kuelekea ukingoni hivyo kuamua abaki au kuachwa.

Hivyo Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa mchezaji huyo bado hajasaini mkataba Mpya huku wakisema wanasubiri ripoti ya Kocha Mkuu, Pablo Franco mwishoni mwa msimu kuona kama atamuhitaji.

Mkataba wa Morrison ndani ya Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa na taarifa kuwa  Yanga inataka kumrudisha kikosini kwao msimu ujao.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, alisema kuwa Morrison bado hajapewa mkataba mpya huku mkataba wake ukiwa ukingoni.


“Lakini hili ni suala la 
benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Pablo ambapo tunasubiri ripoti ya mwisho kutoka kwake kuona kama atamuhitaji basi ataongezewa mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya timu kwa sasa Morrison bado ni mchezaji halali wa Simba na ataendelea kuitumikia timu mpaka hatima yake itakapofahamika mwishoni mwa msimu huu.”

About the author

mzalendoeditor