Featured Kitaifa

DKT.NCHIMBI AENDELEA KUSAKA KURA ZA USHINDI WA KISHINDO ZA DKT.SAMIA JIJINI DAR ES SALAAM

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara wa kampeni,uliofanyika leo Septemba 30,2025 katika uwanja wa Kampala-Gongolamboto,Jimbo la Ukonga wilaya ya ilala,jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika viunga vya Kampala-Ukonga,Dkt.Nchimbi amewahutubia Wananchi huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho ya 2025-2030 yenye kulenga kuimarisha na kupeleka maendeleo kwa Wananchi.

Aidha, baada ya kuhutubia Wananchi,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea
Ubunge wa jimbo la Ukonga,Ndugu Jerry William Silaa, mgombea Ubunge wa jimbo la Kivule Ndugu Dougras Didas Masaburi na Madiwani.

Dkt.Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Mgombea Urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge pamoja na Madiwani.

About the author

Alex Sonna