Featured Kitaifa

RAIS WA AFDB AHITIMISHA ZIARA TANZANIA BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WANAHISA WA AFRICA50.

Written by Alex Sonna

Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, akiagana na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb) (kushoto), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Na. Saidina Msangi, WF, Dar es Salaam.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, amehitimisha ziara yake nchini Tanzania na kuagwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Jukwaa hilo la siku mbili lililofunguliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, liliipatia Tanzania fursa ya kusaini hati tatu za makubaliano ikiwemo hati ya makubaliano ya kujenga kituo kipya cha huduma za usafishaji wa figo, mradi wa kuchakata gesi asilia kuwa gesi kimiminika na makubaliano kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Africa50 ya kuendeleza miundombinu ya usafirishaji wa umeme.

Aidha, Mikutano hiyo iliyokutanisha washiriki wapatao 1,200, imeipatia Tanzania fursa ya kutangaza vivutio vya utalii, uwekezaji na miradi ya kimkakati kwa lengo la kuvutia mitaji na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya miundombinu na hivyo kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Kitaifa wa Miaka Mitano (FYDP IV) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, akiagana na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb) (kushoto), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, akiongozwa kuelekea kupakia ndege na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb) (kulia), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, akiongozwa na na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb) (kushoto), kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.


Picha za matukio mbalimbali wakati Rais wa Benki ya Maendeleo ya AfriKa (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, alipoagana na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb) (kushoto), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Africa50 General Shareholders’ Meeting – GSM and Infra for Africa Forum) iliyofanyika tarehe 5 na 6 Agosti, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

About the author

Alex Sonna