Uncategorized

SH. BILIONI 1.39 KUGHARAMIA UANZISHAJI WA MFUMO JUMUISHI WA KIELETRONIKI WA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII NCHINI.

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akifungua kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwajuma Magwiza,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma’

Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Tullo Masanja akitoa taarifa wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Amina Mfaki, akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.

Mtaalamu wa Mifumo kutoka USAID, Edwin Nyella,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.

……………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imesema zinahitajika Sh.Bilioni 1.39 kugharamia uanzishaji wa mfumo wa jumuishi wa kielektroniki wa huduma za ustawi wa jamii nchini.

Hayo yameelezwa leo April 14,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Dkt.Doroth Gwajima wakati akifunga kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini.

Dkt.Gwajima amesema kuwa  fedha hizo ni kwa ajili ya kusanifu, kutengeneza hadidu za rejea, miundombinu, kuandaa wataalamu wa kutumia mfumo na kusambaza mfumo huo jumuishi nchi nzima.

“Ili kukamilisha mfumo huu pamoja na kuhakikisha unafanya kazi nchi nzima tunahitaji  fedha za kitanzania 1.39 Bilioni” amesema Dkt. Gwajima 

Hata hivyo Waziri Gwajima amewayataka  mashirika ya maendeleo na wadau wote kuunga  mkono juhudi za serikali moja kwa moja kwa kuelekeza rasilimali fedha na ujuzi katika eneo hili ili kuanzisha mfumo Jumuishi wa huduma za Ustawi wa Jamii ili kuboresha utoaji huduma.

Dkt. Gwajima amesema  Wadau pamoja na Serikali wamekuwa wakishirikiana nyakati zote kuanzisha na kuendesha mifumo ya taarifa za huduma za ustawi wa jamii lakini mifumo hiyo imekuwa ikifanyia kazi kundi moja la watoto tu na kuyacha makundi mengin,  hivyo mfumo unaopendekezwa ujumuishe Makundi yote yanayostahili kuwepo.
“Mifumo hii bado ina mapungufu, lazima tufanye kazi kwa pamoja kwani bado haijumuishi huduma zote za Ustawi wa Jamii kwa walengwa wote kama vile wazee na makundi mengine yanayohudumiwa na Ustawi wa jamii”  amesema Dkt. Gwajima
Aidha ameongeza kuwa mifumo iliyopo (MVC- MIS na DCMS) inalenga watoto pekee hivyo kukosa taarifa muhimu kuhusu huduma zinazotolewa kwa makundi mengine. 
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwajuma Magwiza,ameeleza changamoto zilizopo katika mifumo ya awali kuwa ni pamoja na kushindwa kuendana na mahitaji tarajiwa ya Wizara na wadau kwa ujumla ikiwemo kukosa uwezo wa kufuatilia usimamizi wa shauri kwa mtoto mmoja mmoja, hali inayozuia Wizara pamoja na wadau kutumia mfumo huo kutengeneza afua zinazomlenga mnufaika.
“Serikali imeona ipo haja ya kutengeneza mfumo mmoja utakaojumuisha huduma zote za Ustawi wa Jamii ili kurahisisha upatikanaji wa  takwimu na taarifa za huduma zinazotolewa” amesema Bi. Magwiza.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Afyabna Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Amina Mfaki amesema  Serikali kupitia ofisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kukabiliana na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na huduma za msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa ukatili.
”Ametaja baadhi ya shughuli zilizofanywa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kutumia mifumo iliyopo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii 184 katika Halmashauri zote nchini ya kupitia ushirikiano na wadau”amesema Bi.Amina
Kwa upande wake, Mtaalamu wa Mifumo kutoka USAID, Edwin Nyella ameahidi kuunga mkono serikali katika usimikaji wa mfumo huo na uboreshaji wa mifumo iliyopo ya taarifa hizo.
Naye Mtaalam wa Ulinzi wa Mtoto kutoka Shirika la UNICEF Evance Mori amesema wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha huduma kwenye maeneo mbalimbali hususani eneo hilo la taarifa.

About the author

mzalendoeditor