Featured Kimataifa

DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA USAID

Written by mzalendo
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) ukiongozwa na Msaidizi wa Utawala anayesimamia Afrika, Dkt. Monde Muyangwa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Tanzania. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, nchini Marekani na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru na Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha.
 
Ushirikiano wa Tanzania na Marekani umetimiza zaidi ya miaka 50 ambapo makubaliano ya kwanza ya kuanzishwa kwa uhusiano huo yalisainiwa mwaka 1968.

About the author

mzalendo