Featured Michezo

YANGA SC YAZIDI KUINYANYASA SIMBA SC,YAIZAMISHA TENA

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

Baada ya tambo ya Dabi ya Kariakoo hatimaye Leo mzizi wa Fitina umekatwa baada ya Yanga SC kuendeleza ubabe kwa watani zao Simba SC kwa kuwachapa mabao 2_1 Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Kinara wa mabao Stephane Aziz Ki kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 20,na bao la pili likifungwa na Joseph Guede dakika ya 38.

Simba SC walipata bao la kuvutia machozi likifungwa na Fred Michael dakika ya 74,Kwa jumla ya msimu huu Yanga SC imeichapa Simba nje ndani mchezo wa kwanza Mnyama alikufa mabao 5-1.

Kwa ushindi huo Yanga SC wamefikisha pointi 58 wakiendelea kutesa kileleni wakiwa wamecheza mechi 22,Azam FC nafasi ya pili wakiwa na Pointi 51 wakicheza mechi 23 ,huku Simba SC wakishika nafasi ya tatu huku wakicheza mechi 21.

About the author

mzalendoeditor