Mahakama moja nchini Urusi imesema mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich atabakia rumande kabla ya kesi kuzikilizwa hadi Machi 30.
Mahakama hiyo ilitupilia mbali rufaa ya uamuzi wa awali wa kuongeza muda wa kukaa rumande mwandishi wa Jarida la Wall Street hadi tarehe iliyowekwa wakati akikabiliwa na mashtaka ya ujasusi.
Gershkovich na gazeti hilo wamekanusha shutuma hizo. Russia haijatoa ushahidi kuthibitisha mashtaka hayo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia imeeleza Gershkovich anashikiliwa kimakosa.
Gershkovich ambaye ana umri wa miaka 32 alikamatwa wakati akiwa katika safari ya kuripoti katika mji wa Russia wa Yekaterinburg mwezi Machi 2023.
Kadhalika siku ya Jumanne, vyombo vya habari vya Russia viliripoti kuwa mamlaka husika huko Yekaterinburg zilimkamata mwanamke mmoja mwenye uraia pacha wa Marekani na Russia kwa tuhuma za kutoa msaada wa kifedha kwa Ukraine.
“Idara ya Huduma ya Usalama ya Serikali Kuu huko Yekaterinburg ilikandamiza harakati ambazo ni kinyume cha sheria za mkaazi wa Los Angeles mwenye umri wa miaka 33, ambaye ana uraia pacha wa Russia na Marekani,” Shirika la habari la Russia la TASS liliinukuu FSB ikisema hayo.
Msemaji wa Ubalozi wa Marekan mjini Moscow ameiambia VOA inafahamu kuhusu ripoti hizo lakini ilikataa kutoa maoni zaidi kuhusu hali hiyo.