Uncategorized

KAGERA SUGAR,RUVU SHOOTING ZANG’ARA UGENINI LIGI KUU BARA

Written by mzalendoeditor

BAO pekee la Hassan Mwaterema dakika ya 20 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya sita,ikizidiwa pointi moja na Mbeya City inayoendelea kushika nafasi ya tano baada ya timu zote kucheza mechi 18.

Mechi nyingine imechezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenyeji Coastal Union wamechapwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara .
Mabao ya Ruvu Shooting leo yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 19, Haroun Chanongo dakika ya 31 na Samson Joseph dakika ya 79, wakati la Coastal limefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 22.
Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 11, ikizidiwa pointi moja na Coastal baada ya wote kucheza mechi 18.

About the author

mzalendoeditor