Featured Kitaifa

WANAFUNZI WA SEKONDARI PEMBA WAPIGWA MSASA FURSA ZA BAHARI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Stella Katondo akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mkanyageni (hawapo pichani) iliyopo Kisiwani Pemba kuhusu fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani humo.

Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mkanyageni, Jing Shaali akisoma moja ya kipeperushi alichopewa na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Stella Katondo (hayupo pichani), wakati Mkurugenzi na wataalam walipotembelea skuli hiyo iliyopo Kisiwani Pemba kutoa elimu ya kuhusu fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani humo.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Stella Katondo (kushoto) akiteta na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mkanyageni wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea Skuli hiyo iliyopo Kisiwani Pemba, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani humo.

Mwanachama wa Taasisi ya Wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya Usafirishaji Majini kwa Ukanda wa Masharii na Kusini mwa Bara la Afrika (WOMESA), Bi. Raya Khalfan akitoa elimu kuhusu fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho iliyopo Kisiwani Pemba, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani humo.

Nahodha na Mkufunzi kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Haruna Ally akitoa elimu kuhusu fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho iliyopo Kisiwani Pemba, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani humo.

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Moh’d Juma Pindua wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Stella Katondo (hayupo pichani) kuhusu fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani Pemba.

Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Moh’d Juma Pindua akitoa neno la shukran kwa Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za Wzara hizo zilizofika shuleni hapo kutoa elimu ya fursa zilizo katika sekta ndogo ya Bahari, wakati wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya Bahari ambayo kitaifa yanafanyika kisiwani Pemba.

PICHA NA WIZARA YA UCHUKUZI

About the author

mzalendoeditor