Featured Kitaifa

DKT. MAGEMBE ATOA SIKU 7 KWA MKURUGENZI WA GAIRO

Written by mzalendoeditor


Na. Silvia Hyera, Morogoro
Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Grace Magembe amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kuhahakisha ndani ya siku saba fedha za ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ya afya katika Hospitali ya Wilaya Gairo Shilingi Bil. 1.190 zimehamishiwa katika akaunti ya hospitali hiyo.

Kauli hiyo imebainishwa leo Machi 5, 2021 wakati wa majumuisho ya ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo iliyolenga kukagua ubora wa utowaji wa huduma za Afya katika Halmashauri za Gairo na Mvomero Mkoani Morogoro pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ya afya inayoendelea kutekelezwa.

Amesema Dkt. Magembe amesema kupitia mfumo wa malipo FFARS uliopo katika vituo vya kutolea huduma ya Afya unawezesha vituo hivyo kuzisimamia fedha kwa ukaribu na kurahisisha usimamizi wa fedha kwa kuondoa matumizi mabaya ya fedha lakini pia inapelekea ujenzi wa miundombinu kukamilika kwa wakati.

“Nashangaa akauti ya kituo ipo na inafanya kazi lakini fedha bado hazijahamishiwa katika akauti ya kituo, hii inapelekea usheleweshaji wa malipo na miradi kutokamilika kwa wakati” Ameeleza Dkt. Magembe.

Dkt. Magembe amebainisha kuwa Fedha hizo zimepokelewa disema 27, 2021 kwaajili ya ujenzi wa wodi mbili za upasuaji, nyumba tatu za watumishi, jengo la upasuaji pamoja na mochwari ambapo ujenzi huo upo katika hatua ya utelezaji.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Tesha amemshukuru Dkt. Magembe kwa ziara hiyo ambayo imewajengea uwezo katika utendaji kazi na amemhakikishia fedha hizo zinapelekwa katika akaunti husika.

About the author

mzalendoeditor