Featured Kitaifa

CCM KATA YA KILIMANI YAKUTANA KUCHAGUA VIONGOZI KAMATI YA MAADILI NA USALAMA

Written by mzalendoeditor

Na Barnabas Kisengi-DODOMA

HALIMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kata ya kilimani imekutana na kufanya kikao ambacho kilikuwa na agenda moja tu ya kuwachagua viongozi wa kamati ya Maadili na Usalama wa Chama hicho wa Kata ya kilimani.

Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya kilimani Comredi Nathan Chibehe amesema kwa mujibu wa katiba ya chama Cha Mapinduzi na kanuni zake inatekeleza kuundwa kwa Kamati ya Maadili na Usalama ambayo itawezesha kuwasaidia wanachama na Viongozi katika majukumu yao ya kazi za kisiasa katika chama Cha Mapinduzi kata ya kilimani.

Comredi Chibehe amesema kata ya kilimani imejikita kuongeza wanachama na kuhakikisha inaendelea kushika Dola na wanaendelea kujipanga Katika chaguzi zijazo za serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Pamoja na mambo mengine amesema Wajumbe watakao chaguliwa kuongoza kamati hiyo ya Maadili na Usalama wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa haki,uadilifu mkubwa na kuwa na hofu ya mungu.

Akisoma Maelezo ya Uchaguzi wa Kamati hiyo kwa kufuata taratibu za katiba ya CCM na kanuni zake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya kilimani Comredi Rotta Ndimbo amesema kamati ya Maadili na Usalama inaudwa na wajumbe 5 ambapo Mwenyekiti na katibu wanaingia moja kwa moja kwa nafasi zao ambapo Mwenyekiti wa kamati ya Maadili na Usalama atakuwa Mwenyekiti wa kata na Katibu wa CCM kata ndiye atakuwa Katibu wa kamati hiyo na Wajumbe watatu watakao chaguliwa kwa kupigiwa kura na Wajumbe wa Halimashauri kuu kata.

Comredi Rotta Ndimbo ametangaza matokeo baada ya kupigwa kwa kura amesema Wajumbe walio piga kura walikuwa 13 hakuna kura iliyo haribika na idadi ya kura zote halali ni 13.

Ametaja Barnabas Kisengi kuwa amepata kura 12 Kati ya kura 13, huku Tatu Rashidi amepata kura 10 Kati ya kura 13 na Emanuel kabuge amepata kura 10 Kati ya kura 13.

Katibu wa CCM kata ya kilimani amewatangaza Wajumbe hao 3 kuwa hali kuwa Wajumbe wa kamati ya Maadili na Usalama wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya kilimani kuanzia sasa.

Kamati ya Maadili na Usalama wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani itakuwa inamajukumu makubwa na mazito hivyo wazingatie kuhakikisha wanafuata katiba na kanuni za Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza majukumu yao.

About the author

mzalendoeditor