WANANCHI utoka katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha wakipewa elimu juu ya magonjwa ya Saratani na taasisi ya Ocean road katika Kambi inayoendelea katika ya rufaa ya wa Arusha Maunt Meru.
WANANCHI wakisubiri wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya Saratani huduma inayotolewa na taasisi ya Saratani ya Ocean road katika Kambi inayoendelea katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Maunt Meru.
Meneja wa kitengo cha uchunguzi wa Saratani na elimu kwa umma wa taasisi ya Saratani ya Ocean road Dkt Maguha Stephano akitoa elimu ya Saratani kwa madaktari na wauguzi wa hosipitali ya Arusha Lutheran medical center (ALMC)
MADAKTARI na wauguzi wa hosipitali ya Arusha Lutheran medical center wakiwa katika mafunzo ya Saratani yaliyotolewa na taasisi ya Saratani ya Ocean road
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road imefanya uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi na matiti kwa wanawake 351 na Tezi dume kwa wanaume 100 lengo likiwa ni kuwagundua wagonjwa na kuwapatia matibabu ya awali.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja wa kitengo cha uchunguzi wa Saratani na elimu kwa umma Dkt Maguha Stephano katika kambi ya uchunguzi na matibabu unaendelea katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru alisema kuwa tangu kuanza kwa kambi hiyo Machi 6,2023 hadi kufikia Machi 9, 2023 wamewachunguza wanawake 351 ambapo 7 wamegundulika kuwa na mabadiliko ya awali na kupewa matibabu ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi.
Dkr Maguha alisema pia wanawake wanne (4) wamegundulika kuwa na viashiria vya Saratani ya mlango wa Saratani ambapo wanaendelea kufanyiwa vipimo zaidi huku 9 wakigundulika kuwa na vivimbe katika matiti ambapo pia wanaendelea kufanyiwa vipimo ili kubaini kama vivimbe hivyo ni Saratani.
Alifafanua kuwa kati ya wanaume 100 waliofanyiwa uchunguzi wa Tezi dume saba (7) wamekuwa na viashiria na wapo kwenye vipimo zaidi ili kuweza kupata matibu.
Alifafanunua kuwa hali ya Saratani nchini imekuwa ikiongezea siku hadi siku ambapo asilimia 70 ya wagonjwa wanaofika katika taasisi ya Saratani ocean road ni wanawake huku asilimia 75 wanafika wakiwa katika hatua kubwa za ugonjwa.
Alisema kuwa kwa Takwimu za taasisi hiyo za 2021 Saratani ambayo imeongoza kwa wagonjwa wengi kwa upande wa wanawake ni Saratani ya mlango wa kizazi kwa asilimia 47, Saratani ya Matiti kwa asilimia 18 na kufuatiwa na Saratani ya koo la chakula.
Alieleza kwa upande wa wanaume Saratani inayoongoza ni Saratani ya koo la chakula kwa asilimia 18, Saratani ya Tezi dume kwa asilimia 11 na kufuatiwa na Saratani zilizopo maeneo ya kichwani na shingoni ambapo wamekuja mkoa wa Arusha kwa lengo la kugundua Saratani katika hatua za awali ili waweze kupunguza wagonjwa wanaoenda katika taasisi hiyo katika hatua za ugonjwa mkubwa.
“Tumelenga kuwagundua wagonjwa katika hatua za awali zinazotibika kwani Saratani inatibika inapogundulika katika hatua za awali kama unavyoona kati ya wanawake 351 tuliowafanyia uchunguzi tumekuta 7 wanamabadiko ya awali na wameweza kupata matibabu ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi,” Alisema Dkt Maguha.
“Tumekuja kutoa elimu ya magonjwa ya Saratani na kutoa huduma ya awali ya uchunguzi na ugunduzi wa mapema wa Saratani katika hatua za awali bila malipo lakini pia tumeweza kubadilishana uzoefu juu ya Saratani na madaktari wa hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Maunt Meru pamoja na hosipitali ya Arusha Lutheran Medical center (ALMC),” Alisema.
Alisema pia kambi hiyo itarahisisha rufaa za wagonjwa watakaogundulika kuwa Saratani katika hosipitali za mkoa wa Arusha kwenda moja kwa moja katika taasisi ya Saratani ya Ocean road ambapo kambi hiyo imefadhiliwa na benki ya NBC.
Sambamba na hayo pia Alieleza njia za kujinga na Saratani ni kula vyakula ya mboga mboga zaidi, kuepuga ulaji wa mafuta mengi, vyakula vyenye ukungu, kuepuka uzito uliopitiliza, kufanya mazoezi, kupunguza matumizi ya pombe pamoja na kuepuka kutumia bidhaa zinazotengenezwa na tumbaku, kupeleka mabinti kupata chanjo pamoja na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi walifika katika kambi hiyo ya upimaji Janeth Omar alisema ocean road wamekuja kuwasaidia katika vipimo vya Saratani ya titi na shingo ya kizazi kwa wanawake na Tezi dume kwa wanaume ambapo yeye amepima na tayari anajua afya yake.
Neema Joakiam kutoka Njiro alisema kuwa alisikia zoezi hilo katika makundi ya Whatsapp ya akina mama na kuweza kufikia kwani alikuwa anawashwa matiti hali iliyopelekea kuishi kwa wasiwasi na sasa amefanyiwa uchunguzi bure na kugundua kuwa hana tatizo lolote.