Featured Kitaifa

TAWA YAPOKEA MELI NYINGINE YA UTALII KUTOKA NCHINI UFARANSA

Written by mzalendoeditor

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) leo Machi 9, 2023, imepokea meli nyingine ya kimataifa iliyobeba watalii kutoka nchini Ufaransa.

Meli hiyo ya utalii ijulikanayo kama LE JACQUES – CARTIER PONANT, imebeba watalii 125 ambao wametembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya kufanya utalii wa Malikale na fukwe.

Meli ya LE JACQUES – CARTIER PONANT inaendelea na safari katika visiwa vya Pemba na Unguja.

About the author

mzalendoeditor