WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza leo Machi 01, 2021 wakati akieleza mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na waandishi wa habari kilichofanyika jijini Dodoma.
VIONGOZI mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa (hayupo pichani) wakati akieleza mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na waandishi wa habari kilichofanyika leo March 1,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof.Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na waandishi wa habari kilichofanyika leo March 1,2022 jijini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa,akizungumza wakati wa mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwenye kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na waandishi wa habari kilichofanyika leo March 1,2022 jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Na.Hamida Radhaman-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amemtaka Katibu mkuu Profesa Riziki Shemdoe kupeleka maelezo ya kwanini Wakurugenzi wa Halmashauri 19 wamelimbikiza posho za madaraka ya watendaji wa kata miezi mingi bila kuwa na sababu yoyote.
Hayo ameyasema hayo leo March 1,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali wa ngazi tofauti tofauti.
Waziri Bashungwa amesema kunabaadhi ya Halmashauri 19 zimekuwa na shida ambapo zimekuwa hazipeleki posho ya madaraka ya watendaji wa Kata huku akisema fedha hizo sio hisani ni lazima Watendaji wapewe kwani ni maelekezo ya serikali
Aidha amesema Watendaji wa Kata wamekuwa hawakai ofisini na wamekuwa wakuenda kwa wakurugenzi kuomba kupatiwa fedha hizo badala ya kufayashughuli za utendaji wa Kata na kuwahudumia wananchi badala yake wamekuwa watu wakwenda kwa wamurugenzi kuomba fedha tabaia alioomba kuachwa mara moja .
“Kumbukeni kwenye gazi ya Kata watendaji wakata ni watu muhimu sana kwenye kata ndio Mkurugenzikwenye ngazi ya kata ndio wanaokusaidia wewe Mkurugenzi kuleta Maendeleo kwenye Halmashauri yako hivyo nilazima mtambue umuhumu wao na Ndio maana Rais wetu amewawezesha hivyo jambo hilo ni lazima litekelezwe.
Na kuongeza kusema”Wakurugenzi 19 na Halmashauri zenu Mimi nataka kujua kwanini pesa hiyo imelimbikizwa kunawatendaji wengine tangia mwezi Desemba 2021 hadi leo kila siku wanaenda kufuatilia na wakati mwingine mnawajibu vibaya kumbukeni wale ni watumishi wenu wapeni moyo toeni muongozo ili aweze kusimimia maendeleo kwenye kata ,”amesema
Amesema maendeleo yoyote hayafanyiki bila kuwashilikisha watendaji wa Kata hivyo makatibu tawala mkasimiamie hilo kwani hakuna ardhi inayoitwa mkoa wala wilaya yote zipo kwenye Vitongoji Kata na vijiji tuwasamini natuwape miongozo sahihi
Hata hivyo amesema kumekuwepo na tataizo sugu pungufu wa matundu ya vyoo hasa kwenye shule za msingi wakurugenzi na makatibu tawala msisubiri maekekezo yatoke juu mjiongeze msisubiri kauli kutoka juu .
“Tumejengewa madarasa mazuri watoto wetu waweze kusoma bila kubanana hivyo tunasubiri Rais aje aseme na matundu ya vyoo wakati wakurugenzi na na Katibu Tawala mpo,”amesema Bashugwa.
Na kuongeza kuwa “Sasa wakurugezi kwenye bajeti ya fedha ya 2021 /2022 wekeni kiaumbele na mikakati mnakusanya mapato mengi za fedha ya ndani tatueni tatizo hilo la upungufu wa vyoo usisubiri vyombo vya habari vije viebue upungufu huo,”amesema .
Amesema takwimu zinaonyesha upungufu wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi nchi nzima ni zaidi ya 200000 huku upungufu wa matundu ya choo kwa shuke za sekondari ni elfu 44605 .