Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameelezea kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Jenerali Kainerugaba ambaye ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter ukisema kwamba ” “watu wengi (ambao si wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine”.
“Putin yuko sahihi kabisa!” aliongeza.