Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, mchana wa leo Jumanne Machi 01, amezungunza kwa hisia kali na Bunge la Ulaya akiliomba likubali ombi la nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya (European Union) na kushangiliwa kwa nguvu na wabunge hao.
  Rais huyo, ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana kama kiongozi mwenye msimamo na ishara ya ujasiri, amezungumza na wabunge hao mjini Brussels Ubelgiji kwa njia ya video akizungumzia kutoka nchini mwake katika mji wa Kyiv.
“Tutashinda, nina uhakika. Ningependa kuwasikia na nyie mkisema kuwa chaguo la Ukraine la kuwa sehemu ya Ulaya, ni chaguo lenu pia. Tunahitaji kuwa wanachama wa Ulaya. Bila ya nyinyi, Ukraine itakuwa mpweke,” aliliambia bunge  na kugusa hisia za wabunge wengi ambao walisimama na kumpigia makofi kabala na bada ya kuhutubia.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mambo ya sera za nje wa Umoja wa Ulaya, amekaririwa akisema kuwa ombi la Ukraine la kujiunga na umoja huo linaweza kuchukuwa miaka mingi, hivyo ombi lao la kutaka kukubaliwa kujiunga mara moja haliwezekani, hii ni kwa mujibu wa chaneli ya WION English News
Previous articleTANZIA: BABA MZAZI WA GHALIB SAID MOHAMMED AFARIKI DUNIA
Next articleMTOTO WA RAIS MUSEVEN AUNGA MKONO UVAMIZI WA URUSI DHIDI YA UKRAINE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here