Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Jijini Dar es Salaam .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakishuhudia uwekaji saini Mkataba wa makubaliano baina ya Tanzania na DRC, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Kwa upande wa Tanzania, Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na kwa upande wa DRC uliwekwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Christophe Lutundula.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam .