Featured Kitaifa

MSHINDI WA ”M-PESA IMEITIKA” AKABIDHI NYUMBA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.MILIONI 200 NA VODACOM JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Allan Kijazi,akimkabidhi ufunguo Mshindi wa nyumba Rahabu Mwasaga mkazi wa Manyoni mkoani Singida,kupitia kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

……………………………….

 

Na Alex Sonna-DODOMA

KAMPUNI ya simu ya Vodacom nchini imemkabidhi nyumba yenye thamni ya sh.Milioni  200 na samani za ndani zenye thamani ya sh.milioni 60 zilizotolewa na kampuni ya GSM Home kupitia ushirikiano wake na kampuni hiyo mshindi wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika” Bi. Rahabu Mwasaga.

Akizungumza leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Vodacom na M-Pesa Tanzania, Epimack Mbetini,amesema kuwa kampeni hiyo iliyowazawadia washindi 45,105 zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi  millioni 340.

Mbetini amesema kuwa kampuni hiyo imelenga kuboresha maisha ya watu imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa watumiaji wa mtandao huo bila kujali jinsia,dini ,kabila wala hali ya mtu ilimradi tu mteja anatumia mtandao huo kwa kufanya malipo mbalimbali ya kiserikali pamoja na manunuzi ya kawaida.

Amesema katika kaulimbiu ya M-Pesa imeitika kampuni imeweza kutoa zawadi kadhaa kwa vijana kwa kuwapatia bajaji,boda pamoja na zawadi kubwa ambayo ni nyumba huku akieleza kuwa zaidi ya asilimia 99.9 ya washindi ni akina mama.

“Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa ikifanya mashindano kwa watumiaji bora kwa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo

” Kampuni yetu imefanya ubunifu wa kuanzisha mashindano ya M-Pesa imwitika kwa lengo la kutoa zawadi mbalimbali kwa kuinua uchumi wa wateja wetu sambamba na kumuunga kono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kwa kupunguza tozo mbalimbali ambazo zilikuwa zikioekana kuwafanya wateja kukwepa matumizi ya miamala.

“Kutokana hali hiyo wananchi kwa sasa wameanza kufurahia utumiaji wa mtandao kwa kufanya malipo mbalimbali ambapo kwa sasa wateja wanaanza kurejea.

” Sambamba na hilo Vodacom kwa sasa inatoa sh.bilioni.100 kila mwezi kwa ajili ya kuwaongezea mitaji maajenti na mawakala jambo ambalo linaendelea kuwafanya vijana kujikwamua”amesema Epimack.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Allan Kijazi,ameipongeza kampuni ya Vodacom na GSM Home kwa kutoa zawadi hiyo kwa mshindi wa nyumba.

”Kupitia shindano la M-Pesa Imeitika Vodacom imemwezesha mtanzania kumiliki ardhi na nyumba bora na hivyo kuchangia kufanikisha kwa Dira ya Wizara. “Sisi kama serikali tunafurahi kuona huduma za Vodacom zinazolenga kuipeleka Tanzania katika Ulimwengu wa kidijitali hususan katika sekta ya kifedha zinaendelea kushuhudiwa hapa nchini.”amesema Dk.Kijazi

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,amesema kuwa mtiandao ya kijamii imekuwa ikisaidia zaidi kuongeza pato la taifa pamoja na kufanya maendeleo kwa vijana pamoja na kuimarisha uchumi wa watanzania hususani vijana.

“Pamoja na kutoa zawadi mbalimbali lakini huduma ambazo zinatolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania zimekuwa zikisaidia upatikanaji wa huduma kwa rahisi na kuepukana na matumizi ya kutembea na pesa mkonono” amesema Shekimweli.

Mwakilishi wa kampuni ya GSM Home Mkurugenzi Mtendaji Simeon Lawrence amesema GSM Home ushirikiano wao na Vodacom ni wa aina yake na wenye lengo la kukuboresha maisha ya jamii yetu.

“GSM Home ni kampuni inayouza samani za kisasa na bidhaa zingine za nyumbani, tumefurahi sana kushirikiana na kampuni ya Vodacom katika kampeni na tunampongeza mshindi wetu wa leo”amesema Bw.Lawrence

Naye mshindi wa nyumba hiyo Rahabu Mwasaga mkazi wa Manyoni mkoani Singida,ameipongeza Vodacom na kampuni ya GSM Home kwa zawadi hiyo.

“Kwakweli ninayo furaha ya kutosha sijawahi kutegemea kama nitashinda kwa zawadi kubwa kama hii Mimi nilikuwa nikifanya kama mchezo na sijawahi kutumia pesa nyingi bali nilikuwa nikituma pesa kidogo kwa ndugu,kufanya malipo mbalimbali pamoja na kununua bando.

” Nilipigiwa simu na sikuwa mwepesi kuisikiliza kwani nilidhani ni matangazo ya Vodacom lakini niliamua kuweka sauti ya nje na kusikiliza na ndipo nilipobaini kuwa ni sauti halisi ya watu na siyo ile ya kurekodiwa.

Amesema kuwa amekuwa  mteja wa M-Pesa kwa miaka mingi tangu akiwa shule ya sekondari na amefarijika sana kupata mjengo fully furnished. 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Allan Kijazi,akizungumza wakati wa  hafla ya kumkabidhi nyumba mshindi wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa mshindi wa Kampeni ya M-Pesa Imeitika iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Vodacom na M-Pesa Tanzania, Epimack Mbetini,akielezea jinsi wanavyotoa zawadi mbalimbali kutokana na Kampeni zinazofanywa na kampuni hiyo wakati wa hafla ya kumkabidhi nyumba mshindi wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

Mwakilishi wa kampuni ya GSM Home Mkurugenzi Mtendaji Simeon Lawrence,akielezea ushirikiano wao na Vodacom wakati wa hafla ya kumkabidhi nyumba mshindi wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

MKUU wa Kanda ya Kati Vodacom Bw.Joseph Sayi,akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi nyumba mshindi wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Allan Kijazi,akimkabidhi ufunguo Mshindi wa nyumba Rahabu Mwasaga mkazi wa Manyoni mkoani Singida,kupitia kampeni ya “M-Pesa Imeitika” iliyoendeshwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom iliyofanyika leo Septemba 9,2022 katika nyumba za mradi wa shirika la nyumba Tanzania NHC Iyumbu jijini Dodoma.

Mshindi wa nyumba hiyo Bi.Rahabu Mwasaga mkazi wa Manyoni mkoani Singida,akizungumzia jinsi alivyoweza kushinda zawadi hiyo na jinsi alivyotumia pesa mpaka kuibuka mshindi wa nyumba hiyo.

About the author

mzalendoeditor