Featured Kitaifa

WAPAKA RANGI JIJINI DODOMA WABAINISHA CHANGAMOTO WAZOPATA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin- Dodoma

MWENYEKITI wa Wapaka rangi Nyerere Square Mkoani Dodoma Philip Mandoo amewaomba Wateja wao kueshimu na kupunguza vikwazo wanavyovileta katika shughuli yao ya upakaji rangi.

Akizungumza na Mzalendo blog 15 Agosti, 2022 amesema suala hili kwao limekuwa ni changamoto kubwa kutokana na Wateja wengi wamekuwa na dharau pale ambapo wanataja bei yakupaka rangi na baadhi ya wateja wakionyesha dharau ya hali ya juu

“Anaweza akaja Mteja umuhudumie tena anaela ndogo au mwingine anakuja hana ela kabisa na anataka umpake rangi kwa kutumia nguvu kabisa na bora hata awe mstaarabu anakuomba lakini ndio kwanza Mtu anaonyesha dharau njenje”,amesema

” Mtu anadharau biashara huku anahuitaji nao tena anakwambia nishindwe kununua viatu nipake rangi? hii uwa inaumuza Watu wengi na muda mwingine inakatisha tamaa kabisa”.Amesema Mandoo

Aidha amesema kuwa ndoa nyingi za wapaka rangi zinaharibika kutokana na shughuli hiyo ya upakaji rangi.

“Ndoa za wapakarangi wengi zinavunjika kutokana na wivu pia kwasababu sisi ni jinsia ya kiume na wateja wetu ni wakike kuna mteja mwingine anakuja kimtego tu hili apate kitu flani na kama hujitambui unajikuta unaingia kwenye mtego”, amesema

“Juzi tumetoka kusuluhisha kesi hapa ya Mwenzetu Mke wake kaja juu kakuta meseji za mapenzi na jina limeandikwa Mteja kucha, tena hizo meseji ukizisoma unaona kabisa Mteja mwenyewe ndio anamuhitaji kwa nguvu”. Amesema

Ameongezea kwa kusema kuna Wateja wa aina mbili kuna mteja mwingine amekuja siriazi kwaajili ya kupaka rangi lakini na mwingine amekuja kwaajili ya kutaka kitu fulani,

“Na sisi tunajitahidi kutumia akili zetu tusiwapoteze wateja mimi nikiona Mteja anakuja kwaajili ya kitu kingine uwa namkwepa tu ilatusigombane kuepuka kumpoteza na pia kupoteza Wateja Wengine”,amesema

“Unaangalia je nikifanya ntakuwa na sifa gani kwaio tunatumia akili za ziada hili pia tusimpoteze mteja na tunafanya kazi kutokana na jiografia ya Mteja”.Amesema Mandoo

About the author

mzalendoeditor