Burudani Featured

“WASANII WENZANGU WANANISAHAU”-WYSETZ

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

MSANII wa kizazi kipya Bongo fleva Wysetz wiki mbili zilizopita ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram huku amemtagi Msanii wa kike wa muziki Nandy, na kusema kuwa yeye amekuwa akiwaandikia Wasanii wenzake nyimbo kali na kufanya vizuri nje na ndani ya Nchi lakini hao wasanii wamekuwa wanamsahau.

Akizungumza na Mzalendo blog Agosti 15, 2022 amesema ameandika iwasababau anashiriki kuandika nyimbo nyingi za wasanii wenzake lakini wengi wamekuwa wakimsahau

“Nashiriki sana kuandika nyimbo zao lakini wamekuwa wakinisahau hata kwa kunitangaza tu mimi kwangu ni kubwa lakini amna msanii hata mmoja ambae amefanya hivyo

” Na mimi nimeandika kwa kuwakumbusha tua maana labda wanasahau au labda kupitiwa maana sahivi mambo ni mengi”.Amesema Wyse

Ameongezea kwa kusema kuwa hakuwa na nia mbaya ya kuandika vile kwa kutafuta kiki au kuonekana kwa Watu ila aliandika ilikufikisha ujumbe kwa wasanii wanaomfanyia vile.

“Mimi najitambua na ninajua nini nafanya kwaio nilivyoandika vile sio kama niliandika ili nitafute kiki wala kutengeneza skendo hapana ila niliandika ujumbe uwafikie walengwa

“kwasababu siwezi kumfata Mtu mmoja mmoja ila najua ujumbe umewafikia na kama walijisahau basi nimeshawakumbusha kuwa sijapendezwa na hiyo tabia”.Amesema

Wyse ni Mwandishi ambae amewaandikia Wasanii wengi kama Lulu Diva, Offialnandy, Haitham Kim, Hamisa Mobeto, na Wasanii wengine wengi

About the author

mzalendoeditor