Featured • Kitaifa

MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AWASILI MKOANI ARUSHA

Written by Alex Sonna

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius John Ndejembi amewasili Mkoani Arusha leo Jumatatu Oktoba 05, 2026 kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha (KIA) na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Serikali.

Mhe. Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha kwaajili ya kufungua Mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Grand Melia Jijini Arusha, ukiwakutanisha Viongozi na wataalamu zaidi ya 400 kutoka Mataifa 48.

About the author

Alex Sonna