Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wameshiriki kikao cha kujadili Masuala ya Muungano kilichofanyika Zanzibar, leo tarehe 25 Aprili, 2026.
Kikao hicho kimeongozwa na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Saleh Juma Mussa akisaidiwa na Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim J. Yonazi akimwakilisha Katibu Katibu Mkuu Kiongozi (SJMT).
Kikao hicho ni mwanzo wa kikao cha Mawaziri wa SJMT na SMZ kinachotarajiwa kufanyika Aprili 25, 2026 kabla ya kufanyika kwa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ ambayo Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Emmanuel Nchimbi.
Katika kikao cha Makatibu Wakuu, Viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dkt. Islam Seif Salum, Wakurugenzi, Naibu Makatibu Wakuu na wataalamu kutoka Serikali zote mbili.
