Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiongoza Waheshimiwa Wabunge katika kuwapokea wachezaji wa timu ya Serengeti Girl’s chini ya Miaka 17 pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Msaidizi wa Mpambe wa Bunge, Ndg. Ruth Kaijage kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Juni 7, 2022 Jijini Dodoma. Ikiwa ni baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene kutengua kanuni na kuweza kuwaruhusu wachezaji hao kuingia ndani ya Ukumbi huo
Timu hiyo inatarajiwa kwenda kushiriki kombe la dunia chini ya miaka 17 kwa upande wa wanawake Nchini India Mwaka huu, Octoba 2022
Wachezaji wa timu ya Serengeti Girl’s chini ya Miaka 17 wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge Baada ya kufanya vizuri na kupongezwa na Waheshimiwa Wabunge wakiongozwa na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Timu hiyo inatarajiwa kwenda kushiriki kombe la dunia chini ya miaka 17 kwa upande wa wanawake Nchini India Mwaka huu, Octoba 2022
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (koti la Bluu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Serengeti Girl’s pamoja na Waheshimiwa Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, leo Juni 7, 2022, Kulia kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto kwake) na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul (Wapili kushoto)
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)