Featured Kitaifa

OFISI YA RAIS MAENDELEO YA VIJANA YAOMBA BILIONI 35.9 BAJETI 2026/27

Written by Alex Sonna

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka,akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Aprili 20,2026 bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka,akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Aprili 20,2026 bungeni jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA

Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 35.9 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake katika mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa vijana nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka,akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Aprili 20,2026 bungeni Dodoma.

Ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika kugharamia shughuli mbalimbali zinazolenga kuwainua vijana kiuchumi, kijamii na kisiasa, sambamba na utekelezaji wa vipaumbele vilivyowekwa na Serikali.

Mhe. Nanauka amesema kuwa  kiasi kikubwa cha Shilingi trilioni 30.1 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 1.2 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi, huku sehemu kubwa zaidi, takriban Shilingi bilioni 28.8, zikielekezwa kwenye matumizi mengineyo ya uendeshaji wa shughuli za wizara.

Aidha, jumla ya Shilingi bilioni 5.85 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya hizo, Shilingi bilioni 5 ni fedha za ndani zitakazosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwawezesha vijana, huku Shilingi milioni 853 zikitarajiwa kutoka kwa washirika wa maendeleo ili kuunga mkono juhudi hizo.

Kwa ujumla, bajeti hii inaonekana kuwa nguzo muhimu katika safari ya kuwajengea vijana mazingira bora ya kushiriki kikamilifu katika uchumi na maendeleo ya Taifa.

About the author

Alex Sonna