Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki ya Exim ya Marekani, Bw. John Jovanovic, baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi ya Benki hiyo, jijini Washington D.C nchini Marekani kando ya Mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimafaifa-IMF, inayofanyika jijini humo, ambapo walijadili kuongeza ushirikiano ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia miradi mbalimbali ya uzalishaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu, sekta muhimu za madini, nishati, usafiri na usafirishaji na mizigo, dawa na usindikaji wa mazao ya kilimo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Juma Malik Akil (wa tatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Sia Kanza (wa tatu kulia), Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo-TIB, Bw. Deogratius Kwiyukwa (kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania – TCB, Bw. Adam Mihayo (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao na Benki ya Exim ya Marekani, kilichofanyika katika Ofisi ya Benki hiyo, jijini Washington D.C nchini Marekani kando ya Mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimafaifa-IMF, inayofanyika jijini humo, ambapo walijadili kuongeza ushirikiano ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia miradi mbalimbali ya uzalishaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu, sekta muhimu za madini, nishati, usafiri na usafirishaji na mizigo, dawa na usindikaji wa mazao ya kilimo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Sia Kanza, baada ya kikao na Bneki ya EXIM ya Marekani, kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington Nchini Marekani, Kando ya kando ya Mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimafaifa-IMF, inayofanyika jijini humo, ambapo walijadili kuongeza ushirikiano ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia miradi mbalimbali ya uzalishaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu, sekta muhimu za madini, nishati, usafiri na usafirishaji na mizigo, dawa na usindikaji wa mazao ya kilimo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C)
Na Benny Mwaipaja, Washington D.C
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amesema kuwa ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Exim ya Marekani, utachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia miradi mbalimbali ya uzalishaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu, sekta muhimu za madini, nishati, usafiri na usafirishaji na mizigo, dawa na usindikaji wa mazao ya kilimo.
Mhe. Balozi Omar alisema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki ya Exim ya Marekani, Bw. John Jovanovic, Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezomi mwa Mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimafaifa-IMF.
Alisema kuwa malengo ya mkutano huo yalikuwa kuimarisha uhusiano na fursa za ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya EXIM ya Marekani (U.S. EXIM Bank), pamoja na kutafakari njia za ushirikiano wa kiuchumi na kifedha zitakazoongozwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania ya 2050.
“Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050 inasisitiza ukuaji wa sekta binafsi kuwa injini ya ubunifu, uzalishaji, na ajira na kwamba ili kufikia azma hiyo, Serikali inaendelea kufanya mabadiliko ya kisera na kisheria ili kuboresha mazingira ya biashara, kuvutia uwekezaji wa muda mrefu, na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi’ alisema Mhe. Balozi Omar
Mwezi Aprili Mwaka 2023, Wizara ya Fedha, kwa niaba ya Serikali, iliingia makubaliano (MoU) na Benki ya Exim ya Marekani yenye thamani ya dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kuweka misingi ya ushirikiano wa kifedha na kiufundi ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Sekta zinazopewa kipaumbele ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kuwezesha shughuli za kiuchumi ikiwemo madini muhimu, nishati na ufadhili wa miradi ya umeme, Usafiri na usimamizi wa mizigo, dawa na viwanda vya kutengeneza dawa, usindikaji wa bidhaa za kilimo na viwanda vya kusindika chakula.
Kwa upande wake, Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki ya Exim ya Marekani, Bw. John Jovanovic, alisema ushirikiano wa Tanzania na Marekani ni wa kimkakati unaolenga kukuza biashara na uwekezaji kwa faida ya nchi hizo mbili.
Alisema kuwa mwelekeo mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani utajikita katika kutekeleza miradi ya kipaumbele ambayo nchi hizo zitakubaliana huku mtazamo wa Marekani ukiwa ni kuwekeza zaidi katika sekta za madini adimu, kilimo, teknolojia, ujenzi wa miundombinu, viwanda vya dawa pamoja kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza, Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Deogratius Kwiyuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw. Adam Mihayo na maafisa wengine wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Exim ya Marekani.