Featured Kitaifa

TASAC YATOA NENO KWA WAKUU WA WILAYA MKOANI TANGA

Written by mzalendoeditor

Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa
Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na Utalii yanayoendelea
kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
Amina Miruko akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho hayo
Baraka Mashauri ni Afisa kutoka Shirika la Wakati wa Meli Tanzania (TASAC) akizungumza wakati wa maonyesho hayo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

SHIRIKA la Wakala wa
Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Tanga
na viongozi wa Vijiji kutokuvipokea vyombo vya majini ambavyo
havijakidhi vigezo vya kisheria katika maeneo yao kupakia abiria ili nao
waweze kuwa sehemu ya mkakati wa kuhakikisha wanaokoa maisha ya abiria.

Lakini pia kuwa sehemu ya kuhakikisha nao washiriki kudhibiti
safari zinazofanywa na vyombo vinavyotumika kubeba mizigo kupakia
abiria na hivyo kuvunja sheria jambo ambalo linahatarisha maisha.

Wito
huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua wakati
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara
na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema
iwapo viongozi hao watashiriki kwenye suala hilo itakuwa ni mwarobaini
wa kuweza kudhibiti vyombo ambavyo havijaruhusiwa kisheria kufanya
shughuli za kubeba abiria na hivyo kuondokana na matukio mbalimbali
yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajali za majini.

“Lakini pia
niwaambie sisi kama Shirika Kabla hatujachukua sheria inabidi
tuwaelemishe watu hivyo tumejitahidi sana kutoa elimu kwa maeneo sugu ya
watu wanaosafiri kupitia majahazi katika maeneo ya Mkwaja,Kipumbwi na
Pangani kwa wamiliki na manahoida wa vyombo”Alisema

Alisema
kubwa zaidi ni wao kutambua kwamba wana wajibu wa kuhakiksiha hawavunji
sheria na kuhatarisha usalama wa watu wanaotumia vyombo hivyo kwa sababu
havijakidhi vigezo ambavyo vinatakiwa kubeba abiria.

“Tumekuwa
tukiwasiliana na Taasisi za Serikali ikiwemo viongozi wa Vijiji,Wakuu wa
wilaya,Wakuu wa Polisi wilaya na Mkuu wa Mkoa kumpeleka barua
kuwataarifu shughuli zinazofanyika maeneo hayo sio halali na
zinahatarisha maisha ya abiria na hatua zinazofuata ni kuchukua hatua za
kisheria”Alisema

Captain Shalua alisema kwa sababu wanapopewa
leseni zinakuwa na masharti kwamba chombo chako ni cha mizigo na
hakiruhusiwi kubeba abiria hivyo wanapovunja sheria wanachukuliwa hatua
kali ikiwemo kutozwa faini na kuwapeleka mahakamani au vyote viwili kwa
pamoja .

“Kama unavyofahamu eneo la Mwambao wa Bandari ya Tanga
ni kubwa sana na tunategemea viongozi wa serikali za vijiji tusaidiana
nasi kuweza kudhibiti suala hilo kusimamia usalama “Alisema

Hata
hivyo alisema wamiliki wa vyombo vya majini na waendesha vyombo hivyo
wanapaswa kuzingatia masharti ya leseni yao kwa wasafiri kwa kuwaeleza
kwamba hawatakiwi kupanda kwenye majahazi ya mizigo kwa sababu hakuna
mtu anayewalazimisha .

“Hivyo wakipata uelewa kuhusu madhara
yake watafanya maamuzi sahihi ya kuttokupanda vyombo hivyo na hivyo
kusaidia kwa asilimia kubwa kuondokana na changamoto ambazo wanazoweza
kukumbana nazo wawapo safarini”Alisema

Captain Shalua pia
alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kwa na vifaa vya kujiokolea ,kabla
ya kupanda chombo unatakiwa kuangalia kipo kwenye ubora unaostahili na
kinaweza kukusaidia kwenye kusafiri kwenye mazingira salama.


Lakini jambo jingine ni namna bora ya kuvaa vifaa vya kujiokolea na
kwanini lazima kuwepo na vifaa hivyo kwenye chombo kwani ndio sehemu ya
uokozi kuwasaidia pale ajali zinazotokea”Alisema Captain Shalua

Akizungumzia
kuhusu vifaa vya kuzimia moto,Captain Shalua alisema vifaa vya kuzimia
moto vyombo vya majini vingi vinatumia mafuta ya petrol kwa hiyo
wanapenda watumiaji wafahamu namna bora na kifaa gani sahihi cha kuzimia
moto unaowaka na kusababishwa na mafuta.

“Kwani watu wengi
wanakimbia maji na kiuhalisia huwawezi kuzima moto kwa namna hiyo bali
ni vifaa maalumu poda na opovu ili kuweza kizima moto”Alisema

Awali
akizungumza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) Amina Miruko alisema wataendelea kushirikiana na
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoa elimu kwa wananchi
kuhusiana na suala hilo

Alisema pia watahakikisha Bandari Bubu
zilizopo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini zinarasimishwa pale
inapobidi na urasimishaji unaofanyika unakuwa rasmi ikiwemo kufanya
kaguzi za kushtukiza na kupanga.

About the author

mzalendoeditor