Featured Kitaifa

NBAA NA BoT YAWANOA WAHASIBU, BENKI, NA WAKAGUZI ZAIDI YA 400 JUU YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UTOAJI WA TAARIFA NCHINI.

Written by mzalendoeditor

mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Arusha Charles Yamo,akizungumza 

Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu( NBAA) CPA Pius Maneno.

Picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa semina ya huduma za kifedha na utoaji wa taarifa nchini unaendelea mkoani Arusha.

……………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu( NBAA) kwa kushirikiana na benki kuu ya Tanzania(BoT) imetoa semina kwa wahasibu, mabenki, wakaguzi wa fedha bima na kodi juu  ya huduma za kifedha ma utoaji wa taarifa za kifedha   Tanzania.
Akifungua semina hiyo Charles P. Yamo Mkurugenzi wa BoT Arusha kwa niaba ya Profesa Florens Luoga  Gavana wa Benki kuu ya Tanzania alisema ni dhairi kuwa semina zinazoendelea kati ya BoT na NBAA zinachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa kuwa uchumi  unaundwa na sekta ikiwemo  kilimo, mawasiliano ya simu, huduma za kifedha, usafiri ma mengineyo.
“Sekta ya huduma za kifedha inachukuliwa kuwa mojawapo ya sehemu muhimu zaidi ya ukuaji wa uchumi kwani kwa miongo kadhaa ya ukuaji endelevu wa uchumi, Tanzania ilifuzu kutoka hali ya kipato cha chini kwa kuzingatia viwango vya mapato vilivyoanzishwa na Benki ya Dunia na hii inaonyesha ni muhimu kudumisha huduma endelevu za kifedha,” Alisema Yamo.
Alieleza kuwa ni jukumu la sekta ya fedha kuziba pengo la umaskini wa wananchi kwani wanategemea kupata mikopo kwa manunuzi makubwa na kugeukia sekta ya huduma za fedha kwa ajili ya kukopoq na sekta hiyo Ina mchango mkubwa katika kusaidia fedha kwa miradi endelevu na  uwekezaji mpya na fursa za biashara pamoja na  kupunguza hatari zinazohusiana. 
“Kuna dalili za wazi kwamba misingi ya maendeleo endelevu ya kipato kutoka ngazi ya chini,kati na juu  yamewekwa katika nchi yetu na mabadiliko yanawezekana hivyo maendeleo ya sekta hii yanaweza kusaidia ukuaji wa biashara ndogo na za kati kwa kuwapa fursa ya kupata fedha, kukuza ukuaji wa uchumi kupitia uongezaji wa mtaji na maendeleo ya kiteknolojia kwa kuongeza kiwango cha akiba, kuhamasisha na kukusanya akiba, kutoa habari kuhusu uwekezaji,”Alisema.
Alisema Ili kuwa na huduma endelevu na dhabiti za kifedha wanapaswa kuzingatiwa kwa kina kuhusu suala la utoaji taarifa za fedha ambapo wahasibu ni vyanzo vya kuaminika kwani wana uelewa mkubwa zaidi wa tafsiri ya ripoti za fedha ikilinganishwa na wataalamu wengine hivyo taarifa za fedha zilizotayarishwa kwa mujibu wa viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma ni nyenzo muhimu kwa utendakazi mzuri wa masoko.
“Utoaji taarifa duni za fedha utasababisha wawekezaji, wadai, washiriki wa uchumi, wakopeshaji na wengine kupoteza imani na kuweza kukosa ufadhili wa kutosha na kupelekea kupunguza kasi ya uchumi wa nchi, hivyo naamini semina hii italeta ari mpya ya kuboresha ripoti zenu,” Alisisitiza.
Kwa upande wake CPA Pius Maneno mkurugenzi mtendaji wa NBAA alisema kuwa katika semina hiyo Kuna mada kumi na moja ambazo zitawasilishwa na zote zinahusiana na masuala ya benki, fedha kwa maana ya solo ma mitaji, kodi, utawala bora, taarifa za fedha pamoja na majukumu yao kama taaluma ya uhasibu, Benki katika masuala ya utoaji wa taarifa pindi inapotokea fedha haramu.
CPA Maneno alisema kuwa kubwa zaidi ni masuala ya viatarishi kuona ni vitu gani vinasababisha wasifikie malengo yao ya kiofisi au ya nchi lakini pia watatilia mkazo masuala ya matumizi ya mtandao katika kuendeleza uchumi katika kazi zao na jamii kwa ujumla ambapo mkutano huo umeshirikisha watu zaidi ya 400 na itafanyika kwa muda wa siku tatu.
Hata hivyo katika ufunguzi wa semina hiyo wamesisitiza kada hiyo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika  sensa ya watu na makazi mwezi August inafanikiwa kwani wakifanikiwa katika sensa mipango ya uchumi itaenda vizuri, bajeti pamoja na kujiwekea malengo mazuri ya siku zijazo.

About the author

mzalendoeditor