Jumatano, Novemba 25, 2026
HABARI MPYA
Michezo

MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 12 JELA

Na Mwandishi Wetu

MCHEZAJI wa zamani wa  Arsenal na timu ya taifa ya England, Raheem Sterling, amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa kosa la kuendesha gari huku akitumia gesi ya kulevya aina ya Nitrous Oxide, inayojulikana pia kama ‘laughing gas’.

Hukumu hiyo imetolewa Novemba 25, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Basingstoke nchini England, ambapo mchezaji huyo amepangiwa kutumikia kifungo hicho kwa utaratibu wa kusimamishwa (suspended sentence).

Hata hivyo, hukumu hiyo haimaanishi Sterling atakwenda gerezani moja kwa moja, bali atakuwa nje ya gereza kwa masharti kwamba hatakiwi kuvunja sheria katika kipindi cha miezi 18 alichowekewa na mahakama.

Endapo atakiuka masharti hayo au kufanya kosa jingine ndani ya kipindi hicho, anaweza kukabiliwa na hatua za kisheria zitakazoweza kusababisha kutumikia kifungo hicho.

Sterling, ambaye amewahi kucheza katika klabu kubwa za England zikiwemo Liverpool, Manchester City, Chelsea na Arsenal, pia aliitumikia timu ya taifa ya England katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.