Featured • Kitaifa

MAKAMU WA RAIS , AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI

Written by Alex Sonna

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akipokea Zawadi ya Wizara kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kutambua kazi na mchango wake katika Wizara ya Nishati wakati wa hafla fupi na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2026.

….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Jumatano Septemba 09, 2026.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Viongozi na Watendaji hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Watanzania.

Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika hafla fupi ya kuagwa na Wizara ya Nishati iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2026.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akipokea Zawadi ya Wizara kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kutambua kazi na mchango wake katika Wizara ya Nishati wakati wa hafla fupi na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akipokea Zawadi kutoka kwa Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati wakati wa hafla fupi ya kuagwa na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Nishati mara baada ya hafla fupi ya kumuaga, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2026.

About the author

Alex Sonna